Jeremiah 10:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Vinyago hivyo hupambwa kwa fedha kutoka Tarshishi, na dhahabu kutoka Ofiri; kazi ya mafundi stadi na wafua dhahabu. Zimevishwa nguo za samawati na zambarau, zilizofumwa na wafumaji stadi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Huleta fedha iliyofuliwa kutoka Tarshishi na dhahabu kutoka Ufazi. Kile ambacho fundi na sonara wametengeneza huvikwa mavazi ya rangi ya samawi na urujuani: vyote vikiwa vimetengenezwa na mafundi stadi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Iko fedha iliyofuliwa ikawa mabamba, iliyoletwa kutoka Tarshishi, na dhahabu kutoka Ufazi, kazi ya stadi na ya mikono ya mfua dhahabu; mavazi yao ni rangi ya samawi na urujuani; hayo yote ni kazi ya mafundi yao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Vinyago hivyo hupambwa kwa fedha kutoka Tarshishi, na dhahabu kutoka Ofiri; kazi ya mafundi stadi na wafua dhahabu. Zimevishwa nguo za samawati na zambarau, zilizofumwa na wafumaji stadi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Huleta fedha iliyofuliwa kutoka Tarshishi na dhahabu kutoka Ufazi. Kile ambacho fundi na sonara wametengeneza huvikwa mavazi ya rangi ya samawi na urujuani: vyote vikiwa vimetengenezwa na mafundi stadi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Huleta fedha iliyofuliwa kutoka Tarshishi na dhahabu kutoka Ufazi. Kile ambacho fundi na sonara wametengeneza huvikwa mavazi ya rangi ya samawi na urujuani: vyote vikiwa vimetengenezwa na mafundi stadi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Iko fedha iliyofuliwa ikawa mabamba, iliyoletwa kutoka Tarshishi, na dhahabu kutoka Ufazi, kazi ya fundi stadi na ya mikono ya mfua dhahabu; mavazi yao ni rangi ya samawati na urujuani; hayo yote ni kazi ya mafundi wao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Vinyago hivyo hupambwa kwa fedha kutoka Tarshishi, na dhahabu kutoka Ofiri; kazi ya mafundi stadi na wafua dhahabu. Zimevishwa nguo za samawati na zambarau, zilizofumwa na wafumaji stadi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mabati ya fedha yaliyopigwa nyundo huletwa toka Tarsisi, nayo ya dhahabu hutoka Ufazi, mafundi huyatengeneza, kisha mikono ya wafua dhahabu huyaseneza. Mavazi yao ni nguo za kifalme, nyeusi na nyekundu. Yote pia ni kazi za mafundi wazijuao kazi zao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Iko fedha iliyofuliwa ikawa mabamba, iliyoletwa kutoka Tarshishi, na dhahabu kutoka Ufazi, kazi ya stadi na ya mikono ya mfua dhahabu; mavazi yao ni rangi ya samawi na urujuani; hayo yote ni kazi ya mafundi yao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sanamu hizo zinapambwa kwa feza kutoka Tarsisi, na zahabu kutoka Ofiri; zilitengenezwa na wafundi na wafua zahabu. Zimevalishwa nguo nzuri za rangi ya samawi na nyekundu-nyeusi, zilizofumwa na wafundi wa kufuma.