Jeremiah 11:13 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Miungu yako, ewe Yuda imekuwa mingi kama ilivyo miji yako; kama zilivyo nyingi barabara za Yerusalemu, ndivyo zilivyo nyingi madhabahu walizomjengea mungu kinyaa Baali, ili kumfukizia ubani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mnayo miungu mingi kama miji mliyo nayo, ee Yuda, nazo madhabahu mlizozijenga za kumfukizia uvumba huyo mungu wa aibu, Baali ni nyingi kama barabara za Yerusalemu.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana hesabu ya miungu yako, Ee Yuda, ni sawasawa na hesabu ya miji yako; na kama ilivyo hesabu ya njia za Yerusalemu, ndivyo mlivyosimamisha madhabahu za kitu kile cha aibu, madhabahu za kumfukizia Baali uvumba.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Miungu yako, ewe Yuda imekuwa mingi kama ilivyo miji yako; kama zilivyo nyingi barabara za Yerusalemu, ndivyo zilivyo nyingi madhabahu walizomjengea mungu kinyaa Baali, ili kumfukizia ubani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mnayo miungu mingi kama miji mliyo nayo, Ee Yuda, nazo madhabahu mlizozijenga za kufukizia uvumba huyo mungu wa aibu Baali ni nyingi kama barabara za Yerusalemu.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mnayo miungu mingi kama miji mliyo nayo, ee Yuda, nazo madhabahu mlizozijenga za kufukizia uvumba huyo mungu wa aibu Baali ni nyingi kama barabara za Yerusalemu.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana hesabu ya miungu yako, Ee Yuda, ni sawasawa na hesabu ya miji yako; na kama ilivyo hesabu ya njia za Yerusalemu, ndivyo mlivyosimamisha madhabahu za kitu kile cha aibu, madhabahu za kumfukizia Baali uvumba.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Miungu yako, ewe Yuda imekuwa mingi kama ilivyo miji yako; kama zilivyo nyingi barabara za Yerusalemu, ndivyo zilivyo nyingi madhabahu walizomjengea mungu kinyaa Baali, ili kumfukizia ubani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani kama miji yako ilivyo mingi, ndivyo, miungu yako, Yuda, ilivyo mingi nayo. Tena kama barabara za Yerusalemu zilivyo nyingi, ndivyo, palivyo pengi napo, mlipopatengeneza pa kuitambikia iliyo yenye soni, ndipo pa kumvukizia Baali.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana hesabu ya miungu yako, Ee Yuda, ni sawasawa na hesabu ya miji yako; na kama ilivyo hesabu ya njia za Yerusalemu, ndivyo mlivyosimamisha madhabahu za kitu kile cha aibu, madhabahu za kumfukizia Baali uvumba.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Enyi watu wa Yuda, hesabu ya miji yenu ni sawasawa na hesabu ya miungu yenu. Na kama vile barabara zenu za Yerusalema zinavyokuwa nyingi, ndivyo mulivyojenga mazabahu ya haya, ni kusema ya kufukizia ubani kwa mungu Bali.