Jeremiah 11:17 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi niliuotesha huu mzeituni; lakini natangaza maafa dhidi yake kwa sababu ya maovu ambayo watu wa Israeli na Yuda wameyafanya. Wamenikasirisha kwa kumfukizia ubani mungu Baali.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, aliyekupanda, ametamka maafa juu yako, kwa sababu nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda mmefanya maovu na kunikasirisha kwa kumfukizia Baali uvumba.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana Bwana wa majeshi, aliyekupanda, ametamka mabaya juu yako, kwa sababu ya maovu ya nyumba ya Israeli, na ya nyumba ya Yuda, waliyoyatenda juu ya nafsi zao wenyewe kwa kunikasirisha, wakimfukizia Baali uvumba.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi niliuotesha huu mzeituni; lakini natangaza maafa dhidi yake kwa sababu ya maovu ambayo watu wa Israeli na Yuda wameyafanya. Wamenikasirisha kwa kumfukizia ubani mungu Baali.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
BWANA Mwenye Nguvu Zote, aliyekupanda, ametamka maafa kwa ajili yako, kwa sababu nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda mmefanya maovu na kunikasirisha kwa kumfukizia Baali uvumba.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bwana Mwenye Nguvu Zote, aliyekupanda, ametamka maafa kwa ajili yako, kwa sababu nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda mmefanya maovu na kunikasirisha kwa kumfukizia Baali uvumba.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana BWANA wa majeshi, aliyekupanda, ametamka mabaya juu yako, kwa sababu ya maovu ya nyumba ya Israeli, na ya nyumba ya Yuda, waliyoyatenda juu ya nafsi zao wenyewe kwa kunikasirisha, wakimfukizia Baali uvumba.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi niliuotesha huu mzeituni; lakini natangaza maafa dhidi yake kwa sababu ya maovu ambayo watu wa Israeli na Yuda wameyafanya. Wamenikasirisha kwa kumfukizia ubani mungu Baali.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani Bwana Mwenye vikosi aliyekupanda amesema mabaya yatakayokujia kwa ajili ya mabaya, wao wa mlango wa Isiraeli nao wa mlango wa Yuda waliyonifanyizia, wanikasirishe, wakimvukizia Baali.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana BWANA wa majeshi, aliyekupanda, ametamka mabaya juu yako, kwa sababu ya maovu ya nyumba ya Israeli, na ya nyumba ya Yuda, waliyoyatenda juu ya nafsi zao wenyewe kwa kunikasirisha, wakimfukizia Baali uvumba.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mimi Yawe wa majeshi niliuotesha huu muzeituni; lakini sasa ninatangaza hasara juu yake, kwa sababu ya maovu ambayo watu wa Israeli na Yuda wameyafanya. Wamenikasirikisha kwa kumufukizia mungu Bali ubani.