Jeremiah 11:20 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini, ee Mwenyezi-Mungu wa majeshi, wewe unayehukumu kwa haki, unayepima mioyo na akili za watu, unijalie kuona ukiwalipiza kisasi, maana kwako nimekiweka kisa changu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini, Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, wewe uhukumuye kwa haki, uchunguzaye moyo na akili, acha nione ukiwalipiza wao kisasi, kwa maana kwako nimeweka shauri langu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini, Ee Bwana wa majeshi, uhukumuye haki, ujaribuye viuno na moyo, nijalie kuona kisasi chako juu yao; kwa maana nimekufunulia wewe neno langu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini, ee Mwenyezi-Mungu wa majeshi, wewe unayehukumu kwa haki, unayepima mioyo na akili za watu, unijalie kuona ukiwalipiza kisasi, maana kwako nimekiweka kisa changu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini, Ee BWANA Mwenye Nguvu Zote, wewe uhukumuye kwa haki, nawe uchunguzaye moyo na akili, mimi na nione ukiwalipiza wao kisasi, kwa maana kwako nimeweka shauri langu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini, Ee bwana Mwenye Nguvu Zote, wewe uhukumuye kwa haki, nawe uchunguzaye moyo na akili, wacha nione ukiwalipiza wao kisasi, kwa maana kwako nimeweka shauri langu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini, Ee BWANA wa majeshi, uhukumuye kwa haki, ujaribuye fikira na moyo, nijalie kuona kisasi chako juu yao; kwa maana nimekufunulia wewe neno langu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini, ee Mwenyezi-Mungu wa majeshi, wewe unayehukumu kwa haki, unayepima mioyo na akili za watu, unijalie kuona ukiwalipiza kisasi, maana kwako nimekiweka kisa changu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini wewe Bwana Mwenye vikosi, unakata mashauri yaongokayo, unajaribu mafigo na mioyo; na nione, jinsi unavyowalipiza, kwani nimekusukumia wewe shauri langu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini, Ee BWANA wa majeshi, uhukumuye haki, ujaribuye viuno na moyo, nijalie kuona kisasi chako juu yao; kwa maana nimekufunulia wewe neno langu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini, ee Yawe wa majeshi, wewe unayehukumu kwa haki, unayechunguza mioyo na akili za watu, unijalie nione jinsi utakavyowalipiza kisasi, maana ninayaweka maneno yangu kwako.