Jeremiah 11:21 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndiyo maana Mwenyezi-Mungu wa majeshi anacho cha kusema juu ya watu wa Anathothi ambao wanataka kuniua na kuniambia: “Usitoe unabii kwa jina la Mwenyezi-Mungu, la sivyo tutakuua.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Kwa hiyo, hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu kuhusu watu wa Anathothi wanaotafuta uhai wako, wakisema, ‘Usitoe unabii kwa jina la Mwenyezi Mungu, la sivyo utakufa kwa mikono yetu’:
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, kwa hiyo, Bwana asema hivi, juu ya watu wa Anathothi, watakao uhai wako, wakisema, Hutafanya unabii kwa jina la Bwana, usije ukafa kwa mkono wetu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndiyo maana Mwenyezi-Mungu wa majeshi anacho cha kusema juu ya watu wa Anathothi ambao wanataka kuniua na kuniambia: “Usitoe unabii kwa jina la Mwenyezi-Mungu, la sivyo tutakuua.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Kwa hiyo hili ndilo BWANA asemalo kuhusu watu wa Anathothi wale wanaotafuta uhai wako wakisema, ‘Usitoe unabii kwa jina la BWANA la sivyo utakufa kwa mikono yetu’:
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Kwa hiyo hili ndilo bwana asemalo kuhusu watu wa Anathothi wale wanaotafuta uhai wako wakisema, ‘Usitoe unabii kwa jina la bwana, la sivyo utakufa kwa mikono yetu’:
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, kwa hiyo, BWANA asema hivi, juu ya watu wa Anathothi, watakao uhai wako, wakisema, Hutafanya unabii kwa jina la BWANA, usije ukafa kwa mkono wetu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndiyo maana Mwenyezi-Mungu wa majeshi anacho cha kusema juu ya watu wa Anathothi ambao wanataka kuniua na kuniambia: “Usitoe unabii kwa jina la Mwenyezi-Mungu, la sivyo tutakuua.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo Bwana anasema hivyo kwa ajili ya watu wa Anatoti walioitafuta roho yako wakisema: Usitufumbulie kwa Jina la Bwana, usiuawe na mikono yetu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, kwa hiyo, BWANA asema hivi, juu ya watu wa Anathothi, watakao uhai wako, wakisema, Hutafanya unabii kwa jina la BWANA, usije ukafa kwa mkono wetu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo Yawe wa majeshi anasema hivi juu ya watu wa Anatoti ambao wanataka kuniua na kuniambia: Usitutabirie kwa jina la Yawe, kama si vile tutakuua.