Jeremiah 12:1 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ee Mwenyezi-Mungu, wewe ni mwadilifu, ingawa nakulalamikia. Lakini ningependa kutoa hoja zangu mbele yako: Kwa nini waovu hufanikiwa katika mambo yao? Mbona wote wenye hila hustawi?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wewe daima u mwenye haki, Ee Mwenyezi Mungu, niletapo mashtaka mbele yako. Hata hivyo nitazungumza nawe kuhusu hukumu yako: Kwa nini njia ya waovu inafanikiwa? Kwa nini wasio waaminifu wote wanaishi salama?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wewe u mwenye haki, Ee Bwana, nitetapo nawe, lakini nitasema nawe katika habari ya haki. Mbona njia ya wabaya inasitawi? Mbona wote watendao hila wanakaa salama?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ee Mwenyezi-Mungu, wewe ni mwadilifu, ingawa nakulalamikia. Lakini ningependa kutoa hoja zangu mbele yako: Kwa nini waovu hufanikiwa katika mambo yao? Mbona wote wenye hila hustawi?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wewe daima u mwenye haki, Ee BWANA, niletapo daawa mbele yako. Hata hivyo nitazungumza nawe kuhusu hukumu yako: Kwa nini njia ya waovu inafanikiwa? Kwa nini wasiowaaminifu wote wanaishi kwa raha?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wewe daima u mwenye haki, Ee bwana, niletapo mashtaka mbele yako. Hata hivyo nitazungumza nawe kuhusu hukumu yako: Kwa nini njia ya waovu inafanikiwa? Kwa nini wasio waaminifu wote wanaishi kwa raha?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wewe u mwenye haki, Ee BWANA, nitetapo nawe, lakini nitasema nawe katika habari ya haki. Mbona njia ya wabaya inasitawi? Mbona wote watendao hila wanakaa salama?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ee Mwenyezi-Mungu, wewe ni mwadilifu, ingawa nakulalamikia. Lakini ningependa kutoa hoja zangu mbele yako: Kwa nini waovu hufanikiwa katika mambo yao? Mbona wote wenye hila hustawi?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wewe Bwana hushinda, nikiulizana wa wewe; lakini na tusemeane hukumu zipasazo! Mbona njia zao wasiokucha huendelea vema, nao wadanganyifu wanaodanganya hutengemana?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wewe u mwenye haki, Ee BWANA, nitetapo nawe, lakini nitasema nawe katika habari ya haki. Mbona njia ya wabaya inasitawi? Mbona wote watendao hila wanakaa salama?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ee Yawe, wewe ni mwenye haki, ingawa nitakushitaki. Lakini ningependa nibishane nawe juu ya mambo ya haki: Kwa nini waovu wanafanikiwa katika mambo yao? Mbona wote wanaodanganya wanastawi?