Jeremiah 12:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini wewe ee Mwenyezi-Mungu wanijua; wayathibiti maelekeo yangu kwako. Uwaokote hao kama kondoo wa kuchinjwa, watenge kwa ajili ya wakati wa kuuawa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hata hivyo unanijua mimi, Ee Mwenyezi Mungu; unaniona na kuyachunguza mawazo yangu kukuhusu wewe. Wakokote kama kondoo wanaoenda kuchinjwa! Watenge kwa ajili ya siku ya kuchinjwa!
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini wewe, Bwana, wanijua; umeniona, umeujaribu moyo wangu, jinsi unavyokuelekea; uwakokote kama kondoo waendao kuchinjwa, ukawaweke tayari kwa siku ya kuchinjwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini wewe ee Mwenyezi-Mungu wanijua; wayathibiti maelekeo yangu kwako. Uwaokote hao kama kondoo wa kuchinjwa, watenge kwa ajili ya wakati wa kuuawa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hata hivyo unanijua mimi, Ee BWANA; unaniona na kuyachunguza mawazo yangu kukuhusu wewe. Wakokote kama kondoo wanaokwenda kuchinjwa! Watenge kwa ajili ya siku ya kuchinjwa!
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hata hivyo unanijua mimi, Ee bwana; unaniona na kuyachunguza mawazo yangu kukuhusu wewe. Wakokote kama kondoo wanaokwenda kuchinjwa! Watenge kwa ajili ya siku ya kuchinjwa!
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini wewe, BWANA, wanijua; umeniona, umeujaribu moyo wangu, jinsi unavyokuelekea; uwakokote kama kondoo waendao kuchinjwa, ukawaweke tayari kwa siku ya kuchinjwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini wewe ee Mwenyezi-Mungu wanijua; wayathibiti maelekeo yangu kwako. Uwaokote hao kama kondoo wa kuchinjwa, watenge kwa ajili ya wakati wa kuuawa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nawe Bwana unanijua, ukaniona, ukanijaribu moyo wangu, kama u kwako. Wakamate kama kondoo wa kuchinjwa, kawachagulie, wawe tayari siku ya kuchinjwa!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini wewe, BWANA, wanijua; umeniona, umeujaribu moyo wangu, jinsi unavyokuelekea; uwakokote kama kondoo waendao kuchinjwa, ukawaweke tayari kwa siku ya kuchinjwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini wewe ee Yawe unanijua; umeniona na kunipima. Unajua namna ninavyokutegemea, uwatayarishe kwa ajili ya siku ya kuuawa.