Jeremiah 13:17 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini kama msiponisikiliza, moyo wangu utalia machozi faraghani, kwa sababu ya kiburi chenu. Nitalia kwa uchungu na kububujika machozi, kwa kuwa watu wa Mwenyezi-Mungu wametekwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini kama hamtasikiliza, nitalia sirini kwa ajili ya kiburi chenu; macho yangu yatalia kwa uchungu, yakitiririka machozi, kwa sababu kundi la kondoo la Mwenyezi Mungu litachukuliwa mateka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bali kama hamtaki kusikia, roho yangu italia kwa siri, kwa sababu ya kiburi chenu; na jicho langu litalia sana na kutoka machozi mengi, kwa kuwa kundi la Bwana limechukuliwa hali ya kufungwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini kama msiponisikiliza, moyo wangu utalia machozi faraghani, kwa sababu ya kiburi chenu. Nitalia kwa uchungu na kububujika machozi, kwa kuwa watu wa Mwenyezi-Mungu wametekwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini kama hamtasikiliza, nitalia sirini kwa ajili ya kiburi chenu; macho yangu yatalia kwa uchungu, yakitiririka machozi, kwa sababu kundi la kondoo na mbuzi la BWANA litachukuliwa mateka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini kama hamtasikiliza, nitalia sirini kwa ajili ya kiburi chenu; macho yangu yatalia kwa uchungu, yakitiririka machozi, kwa sababu kundi la kondoo la bwana litachukuliwa mateka.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Bali kama hamtaki kusikia, roho yangu italia kwa siri, kwa sababu ya kiburi chenu; na jicho langu litalia sana na kutoka machozi mengi, kwa kuwa kundi la BWANA limechukuliwa mateka.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini kama msiponisikiliza, moyo wangu utalia machozi faraghani, kwa sababu ya kiburi chenu. Nitalia kwa uchungu na kububujika machozi, kwa kuwa watu wa Mwenyezi-Mungu wametekwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini msiposikia, roho yangu itayalilia majivuno yenu mafichoni, nayo macho yangu yatachuruzika machozi pasipo kukoma, kwa kuwa kundi la Bwana limetekwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Bali kama hamtaki kusikia, roho yangu italia kwa siri, kwa sababu ya kiburi chenu; na jicho langu litalia sana na kutoka machozi mengi, kwa kuwa kundi la BWANA limechukuliwa hali ya kufungwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na kama musiponisikiliza, moyo wangu utalia machozi kwenye uficho, kwa sababu ya kiburi chenu. Nitalia kwa uchungu na kutoa machozi, maana watu wa Yawe wanapelekwa katika uhamisho.