Jeremiah 13:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ikawa, baada ya siku nyingi, Mwenyezi-Mungu akaniambia, “Nenda kwenye mto Eufrate, ukakichukue kile kikoi nilichokuamuru ukifiche huko.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada ya siku nyingi Mwenyezi Mungu akaniambia, “Nenda sasa Frati ukauchukue ule mkanda niliokuambia uufiche huko.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata ikawa, baada ya siku nyingi, Bwana akaniambia, Ondoka, enenda mpaka mto Frati, ukautwae ule mshipi, niliokuamuru kuuficha huko.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ikawa, baada ya siku nyingi, Mwenyezi-Mungu akaniambia, “Nenda kwenye mto Eufrate, ukakichukue kile kikoi nilichokuamuru ukifiche huko.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baada ya siku nyingi BWANA akaniambia, “Nenda sasa Eufrati na ukauchukue ule mkanda niliokuambia uufiche huko.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baada ya siku nyingi bwana akaniambia, “Nenda sasa Frati ukauchukue ule mkanda niliokuambia uufiche huko.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hata ikawa, baada ya siku nyingi, BWANA akaniambia, Ondoka, nenda mpaka mto Frati, ukakitwae kile kitambaa, nilichokuamuru kukificha huko.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ikawa, baada ya siku nyingi, Mwenyezi-Mungu akaniambia, “Nenda kwenye mto Eufrate, ukakichukue kile kikoi nilichokuamuru ukifiche huko.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikawa, siku nyingi zilipopita, ndipo, Bwana aliponiambia: Inuka, uende Furati, uuchukue kule mshipi, niliokuagiza kuuficha huko.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata ikawa, baada ya siku nyingi, BWANA akaniambia, Ondoka, enenda mpaka mto Frati, ukautwae ule mshipi, niliokuamuru kuuficha huko.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kulipokwisha kupita siku nyingi, Yawe akaniambia: Kwenda kwenye muto Furati, utwae ule mukaba niliokuamuru kuuficha huko.