Jeremiah 13:7 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, nikaenda kwenye mto Eufrate, nikachimbua na kukitoa kile kikoi mahali nilipokuwa nimekificha. Nilipokitoa, nilishangaa kukiona kuwa kilikuwa kimeharibika kabisa; kilikuwa hakifai tena.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo nikaenda Frati na kuuchimbua ule mkanda kutoka pale nilipokuwa nimeuficha, lakini sasa ulikuwa umeharibika na haufai tena kabisa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo nikaenda mpaka mto Frati, nikachimba, nikautwaa ule mshipi katika mahali pale nilipouficha; na tazama, mshipi ulikuwa umeharibika, haukufaa tena kwa lo lote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, nikaenda kwenye mto Eufrate, nikachimbua na kukitoa kile kikoi mahali nilipokuwa nimekificha. Nilipokitoa, nilishangaa kukiona kuwa kilikuwa kimeharibika kabisa; kilikuwa hakifai tena.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo nikaenda Eufrati na kuuchimbua ule mkanda kutoka pale nilipokuwa nimeuficha, lakini sasa ulikuwa umeharibika na haufai tena kabisa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo nikaenda Frati na kuuchimbua ule mkanda kutoka pale nilipokuwa nimeuficha, lakini sasa ulikuwa umeharibika na haufai tena kabisa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo nikaenda mpaka mto Frati, nikachimba, nikakitwaa kile kitambaa katika mahali pale nilipokificha; na tazama, kitambaa kilikuwa kimeharibika, hakikufaa tena kwa lolote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, nikaenda kwenye mto Eufrate, nikachimbua na kukitoa kile kikoi mahali nilipokuwa nimekificha. Nilipokitoa, nilishangaa kukiona kuwa kilikuwa kimeharibika kabisa; kilikuwa hakifai tena.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nikaenda Furati, nikauchimbua, nikauchukua ule mshipi mahali hapo, nilipouficha; lakini nilipoutazama ule mshipi, ulikuwa umeharibika, haukufaa kitu cho chote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo nikaenda mpaka mto Frati, nikachimba, nikautwaa ule mshipi katika mahali pale nilipouficha; na tazama, mshipi ulikuwa umeharibika, haukufaa tena kwa lo lote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, nikaenda kwenye muto Furati, nikachimbua na kuuondoa ule mukaba pahali nilipokuwa nimeuficha. Nilipouondoa, niliona kwamba ulikuwa umeharibika kabisa; nao ulikuwa haufai tena.