Jeremiah 14:17 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hivi ndivyo utakavyowaambia: Laiti macho yangetoa machozi kutwa kucha, wala yasikome kububujika, maana, watu wangu wamejeruhiwa vibaya, wamepata pigo kubwa sana.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Nena nao neno hili: “ ‘Macho yangu na yatiririkwe na machozi usiku na mchana bila kukoma; kwa kuwa binti yangu aliye bikira, yaani watu wangu, amepata jeraha baya, pigo la kuangamiza.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nawe utawaambia neno hili, Macho yangu na yatiririke machozi, usiku na mchana, wala yasikome; kwa maana bikira, binti ya watu wangu, amevunjika mavunjiko makuu, kwa jeraha isiyoponyeka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hivi ndivyo utakavyowaambia: Laiti macho yangetoa machozi kutwa kucha, wala yasikome kububujika, maana, watu wangu wamejeruhiwa vibaya, wamepata pigo kubwa sana.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Nena nao neno hili: “ ‘Macho yangu na yatiririkwe na machozi usiku na mchana bila kukoma; kwa kuwa binti yangu aliye bikira, yaani watu wangu, amepata jeraha baya, pigo la kuangamiza.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Nena nao neno hili: “ ‘Macho yangu na yatiririkwe na machozi usiku na mchana bila kukoma; kwa kuwa binti yangu aliye bikira, yaani watu wangu, amepata jeraha baya, pigo la kuangamiza.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nawe utawaambia neno hili, Macho yangu na yatiririke machozi, usiku na mchana, wala yasikome; kwa maana bikira, binti ya watu wangu, amevunjika mavunjiko makuu, kwa jeraha lisiloponyeka.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hivi ndivyo utakavyowaambia: Laiti macho yangetoa machozi kutwa kucha, wala yasikome kububujika, maana, watu wangu wamejeruhiwa vibaya, wamepata pigo kubwa sana.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nawe na uwaambie neno hili: Macho yangu yanachuruzika machozi usiku na mchana, hayakomi, kwani wanawali walio wazaliwa wa ukoo wangu wamevunjika mavunjiko makuu, ni pigo lisilopona kabisa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nawe utawaambia neno hili, Macho yangu na yatiririke machozi, usiku na mchana, wala yasikome; kwa maana bikira, binti ya watu wangu, amevunjika mavunjiko makuu, kwa jeraha isiyoponyeka.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hivi ndivyo utakavyowaambia: Heri macho yangetoa machozi usiku na muchana, wala yasikome kutiririka, maana, watu wangu wamepata hasara kubwa, wameumizwa kidonda kikubwa sana.