Jeremiah 14:22 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Je miungu ya uongo ya mataifa yaweza kuleta mvua? Au, je, mbingu zaweza kutoa manyunyu? Je, si wewe ee Mwenyezi-Mungu uliye Mungu wetu? Tunakuwekea wewe tumaini letu, maana wewe unayafanya haya yote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Je, kuna sanamu batili yoyote ya mataifa iwezayo kuleta mvua? Je, anga peke yake zinaweza kuleta mvua? La hasha! Ni wewe peke yako, Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wetu. Kwa hiyo tumaini letu liko kwako, kwa kuwa wewe ndiwe ufanyaye haya yote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Je! Katika vitu vya ubatili vya mataifa, kiko kitu kiwezacho kuleta mvua? Je! Mbingu zaweza kutoa manyunyu? Je! Si wewe, Ee Bwana, Mungu wetu? Kwa sababu hiyo tutakungoja; kwa kuwa wewe umevifanya vitu hivi vyote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Je miungu ya uongo ya mataifa yaweza kuleta mvua? Au, je, mbingu zaweza kutoa manyunyu? Je, si wewe ee Mwenyezi-Mungu uliye Mungu wetu? Tunakuwekea wewe tumaini letu, maana wewe unayafanya haya yote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Je, kuna sanamu yo yote isiyofaa kitu ya mataifa iwezayo kuleta mvua? Je, anga peke yake zaweza kutoa mvua? La hasha, ni wewe peke yako, Ee BWANA, Mungu wetu. Kwa hiyo tumaini letu liko kwako, kwa kuwa wewe ndiwe ufanyaye haya yote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Je, kuna sanamu yoyote isiyofaa kitu ya mataifa iwezayo kuleta mvua? Je, anga peke yake zaweza kutoa mvua? La hasha, ni wewe peke yako, Ee bwana, Mungu wetu. Kwa hiyo tumaini letu liko kwako, kwa kuwa wewe ndiwe ufanyaye haya yote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Je! Katika vitu vya ubatili vya mataifa, kiko kitu kiwezacho kuleta mvua? Je! Mbingu zaweza kutoa manyunyu? Je! Si wewe, Ee BWANA, Mungu wetu? Kwa sababu hiyo tutakungoja; kwa kuwa wewe umevifanya vitu hivi vyote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Je miungu ya uongo ya mataifa yaweza kuleta mvua? Au, je, mbingu zaweza kutoa manyunyu? Je, si wewe ee Mwenyezi-Mungu uliye Mungu wetu? Tunakuwekea wewe tumaini letu, maana wewe unayafanya haya yote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Je? Katika miungu ya wamizimu isiyo kitu imo iwezayo kunyesha mvua? Au ni mbingu zitoazo zenyewe manyunyu tu? Si wewe, Bwana Mungu wetu? Kwa hiyo tunakungojea, kwani wewe ndiwe ayafanyaye haya yote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Je! Katika vitu vya ubatili vya mataifa, kiko kitu kiwezacho kuleta mvua? Je! Mbingu zaweza kutoa manyunyu? Je! Si wewe, Ee BWANA, Mungu wetu? Kwa sababu hiyo tutakungoja; kwa kuwa wewe umevifanya vitu hivi vyote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katikati ya miungu ya uongo ya mataifa nani anayeweza kunyesha mvua? Au, ni mbingu ndiyo inaweza kutoa manyunyu? Si ni wewe ee Yawe, Mungu wetu? Tunakuwekea wewe tumaini letu, maana ni wewe unayefanya haya yote.