Jeremiah 14:7 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Nao watu wanasema: Ingawa dhambi zetu zashuhudia dhidi yetu, utusaidie ee Mwenyezi-Mungu kwa heshima ya jina lako. Maasi yetu ni mengi, tumetenda dhambi dhidi yako.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ingawa dhambi zetu zinashuhudia dhidi yetu, Ee Mwenyezi Mungu, tenda jambo kwa ajili ya jina lako. Kwa kuwa kukengeuka kwetu ni kukubwa, nasi tumetenda dhambi dhidi yako.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ijapokuwa maovu yetu yanatushuhudia, lakini utende wewe kwa ajili ya jina lako, Ee Bwana, maana kurudi nyuma kwetu ni kwingi; tumekutenda dhambi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Nao watu wanasema: Ingawa dhambi zetu zashuhudia dhidi yetu, utusaidie ee Mwenyezi-Mungu kwa heshima ya jina lako. Maasi yetu ni mengi, tumetenda dhambi dhidi yako.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ingawa dhambi zetu zinashuhudia juu yetu, Ee BWANA, tenda jambo kwa ajili ya jina lako. Kwa kuwa kukengeuka kwetu ni kukubwa, nasi tumetenda dhambi dhidi yako.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ingawa dhambi zetu zinashuhudia juu yetu, Ee bwana, tenda jambo kwa ajili ya jina lako. Kwa kuwa kukengeuka kwetu ni kukubwa, nasi tumetenda dhambi dhidi yako.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ijapokuwa maovu yetu yanatushuhudia, lakini utende wewe kwa ajili ya jina lako, Ee BWANA, maana kurudi nyuma kwetu ni kwingi; tumekutenda dhambi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Nao watu wanasema: Ingawa dhambi zetu zashuhudia dhidi yetu, utusaidie ee Mwenyezi-Mungu kwa heshima ya jina lako. Maasi yetu ni mengi, tumetenda dhambi dhidi yako.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kweli manza, tulizozikora, zimetusuta; lakini, Bwana, yafanye yalipasayo Jina lako! Kwani tumekuacha mara nyingi, tukarudi nyuma, tumekukosea kweli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ijapokuwa maovu yetu yanatushuhudia, lakini utende wewe kwa ajili ya jina lako, Ee BWANA, maana kurudi nyuma kwetu ni kwingi; tumekutenda dhambi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nao watu wanasema: Ingawa zambi zetu zinatoa ushuhuda juu yetu, utusaidie ee Yawe kwa ajili ya heshima ya jina lako. Maasi yetu ni mengi, tumetenda zambi mbele yako.