Jeremiah 14:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Utakuwaje kama mtu uliyechanganyikiwa, kama shujaa asiyeweza kusaidia mtu? Lakini wewe ee Mwenyezi-Mungu, u pamoja nasi; sisi twaitwa kwa jina lako, usituache.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mbona unakuwa kama mtu aliyeshtukizwa, kama shujaa asiye na uwezo wa kuokoa? Wewe uko katikati yetu, Ee Mwenyezi Mungu, nasi tunaitwa kwa jina lako; usituache!
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa nini wewe umekuwa kama mtu aliyesituka, kama shujaa asiyeweza kuokoa? Lakini wewe, Bwana, u katikati yetu, nasi tunaitwa kwa jina lako; usituache.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Utakuwaje kama mtu uliyechanganyikiwa, kama shujaa asiyeweza kusaidia mtu? Lakini wewe ee Mwenyezi-Mungu, u pamoja nasi; sisi twaitwa kwa jina lako, usituache.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mbona unakuwa kama mtu aliyeshtukizwa, kama shujaa asiye na uwezo wa kuokoa? Wewe uko katikati yetu, Ee BWANA, nasi tunaitwa kwa jina lako; usituache!
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mbona unakuwa kama mtu aliyeshtukizwa, kama shujaa asiye na uwezo wa kuokoa? Wewe uko katikati yetu, Ee bwana, nasi tunaitwa kwa jina lako; usituache!
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa nini wewe umekuwa kama mtu aliyeshtuka, kama shujaa asiyeweza kuokoa? Lakini wewe, BWANA, u katikati yetu, nasi tunaitwa kwa jina lako; usituache.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Utakuwaje kama mtu uliyechanganyikiwa, kama shujaa asiyeweza kusaidia mtu? Lakini wewe ee Mwenyezi-Mungu, u pamoja nasi; sisi twaitwa kwa jina lako, usituache.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mbona unataka kuwa kama mtu aliyeshindwa au kama fundi wa vita asiyeweza kuokoa? Wewe, Bwana, uko kwetu katikati, nasi huitwa kwa Jina lako, usituache!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa nini wewe umekuwa kama mtu aliyesituka, kama shujaa asiyeweza kuokoa? Lakini wewe, BWANA, u katikati yetu, nasi tunaitwa kwa jina lako; usituache.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Namna gani unakuwa kama mutu aliyechanganyikiwa, kama shujaa asiyeweza kusaidia mutu? Ingawa hivyo wewe ee Yawe unakaa katikati yetu; nasi tunajulikana kwa jina lako, usituache.