Jeremiah 15:18 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa nini mateso yangu hayaishi? Mbona jeraha langu haliponi, wala halitaki kutibiwa? Ama kweli umenidanganya, kama kijito cha maji ya kukaukakauka!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa nini maumivu yangu hayakomi, na jeraha langu ni la kuhuzunisha, wala haliponyeki? Je, utakuwa kwangu kama kijito cha udanganyifu, kama chemchemi iliyokauka?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mbona maumivu yangu ni ya daima, na jeraha yangu haina dawa, inakataa kuponywa? Je! Yamkini wewe utakuwa kwangu kama kijito kidanganyacho, na kama maji yasiyodumu?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa nini mateso yangu hayaishi? Mbona jeraha langu haliponi, wala halitaki kutibiwa? Ama kweli umenidanganya, kama kijito cha maji ya kukaukakauka!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa nini maumivu yangu hayakomi na jeraha langu ni la kuhuzunisha wala haliponyeki? Je, utakuwa kwangu kama kijito cha udanganyifu, kama chemchemi iliyokauka?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa nini maumivu yangu hayakomi, na jeraha langu ni la kuhuzunisha, wala haliponyeki? Je, utakuwa kwangu kama kijito cha udanganyifu, kama chemchemi iliyokauka?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mbona maumivu yangu ni ya daima, na jeraha langu halina dawa, linakataa kuponywa? Je! Yamkini wewe utakuwa kwangu kama kijito kidanganyacho, na kama maji yasiyodumu?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa nini mateso yangu hayaishi? Mbona jeraha langu haliponi, wala halitaki kutibiwa? Ama kweli umenidanganya, kama kijito cha maji ya kukaukakauka!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mbona maumivu yangu hayakomi? Mbona kidonda changu ni kibaya sana kwa kukataa kupona? Utaniwia kama kijito kidanganyacho au kama maji yasiyotegemeka?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mbona maumivu yangu ni ya daima, na jeraha yangu haina dawa, inakataa kuponywa? Je! Yamkini wewe utakuwa kwangu kama kijito kidanganyacho, na kama maji yasiyodumu?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa nini mateso yangu hayaishi? Mbona kidonda changu hakiponi nacho hakitaki kutunzwa? Kama vile kijito chenye kukaukakauka, kisivyoweza kutumainiwa, ndivyo wewe umekuwa kwangu!