Jeremiah 15:19 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu akajibu: “Kama ukinirudia nitakurudishia hali ya kwanza, nawe utanitumikia tena. Kama ukisema maneno ya maana na sio ya upuuzi, basi utakuwa msemaji wangu. Watu watakuja kujumuika nawe, wala sio wewe utakayekwenda kwao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: “Ukitubu, nitakurejesha ili uweze kunitumikia; ukinena maneno yenye maana, wala si ya upuzi, utakuwa mnenaji wangu. Watu hawa ndio watakaokugeukia, wala si wewe utakayewageukia wao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa sababu hiyo Bwana asema hivi, Ukirudi, ndipo mimi nitakapokurejeza, upate kusimama mbele zangu; nawe ukitoa kilicho cha thamani katika kilicho kibovu, utakuwa kama kinywa changu; nao watakurudia wewe, bali hutawarudia wao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu akajibu: “Kama ukinirudia nitakurudishia hali ya kwanza, nawe utanitumikia tena. Kama ukisema maneno ya maana na sio ya upuuzi, basi utakuwa msemaji wangu. Watu watakuja kujumuika nawe, wala sio wewe utakayekwenda kwao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo hili ndilo asemalo BWANA: “Kama ukitubu, nitakurejeza ili uweze kunitumikia; kama ukinena maneno yenye maana, wala si ya upuzi, utakuwa mnenaji wangu. Watu hawa ndio watakaokugeukia, wala si wewe utakayewageukia wao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo hili ndilo asemalo bwana: “Kama ukitubu, nitakurejeza ili uweze kunitumikia; kama ukinena maneno yenye maana, wala si ya upuzi, utakuwa mnenaji wangu. Watu hawa ndio watakaokugeukia, wala si wewe utakayewageukia wao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa sababu hiyo BWANA asema hivi, Ukirudi, ndipo mimi nitakapokurejesha, upate kusimama mbele zangu; nawe ukitoa kilicho cha thamani katika kilicho kibovu, utakuwa kama kinywa changu; nao watakurudia wewe, bali hutawarudia wao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu akajibu: “Kama ukinirudia nitakurudishia hali ya kwanza, nawe utanitumikia tena. Kama ukisema maneno ya maana na sio ya upuuzi, basi utakuwa msemaji wangu. Watu watakuja kujumuika nawe, wala sio wewe utakayekwenda kwao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kweli hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Utakaporudi, ndipo, nitakapokurudisha, usimame tena usoni pangu! Nao wapaswao na macheo utakapowatoa kwao wasiofaa, ndipo, utakapokuwa kama kinywa changu, ndipo, wale watakaporudi upande wako, wewe usiporudi upande wao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa sababu hiyo BWANA asema hivi, Ukirudi, ndipo mimi nitakapokurejeza, upate kusimama mbele zangu; nawe ukitoa kilicho cha thamani katika kilicho kibovu, utakuwa kama kinywa changu; nao watakurudia wewe, bali hutawarudia wao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, Yawe akasema hivi: Kama ukinirudilia, nitakurudisha katika hali yako ya mbele, nawe utanitumikia tena. Kama ukisema maneno ya maana, yasiyokuwa ya upuuzi, basi utakuwa musemaji wangu. Watu watakufikia wewe, wala si wewe utakayehitaji kuwaendea.