Jeremiah 15:2 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Na wakikuuliza, ‘Twende wapi?’ wewe utawajibu kuwa mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Waliopangiwa kufa kwa maradhi, watakufa kwa maradhi; waliopangiwa kufa kwa upanga, watakufa kwa upanga; waliopangiwa kufa kwa njaa, watakufa kwa njaa; na waliopangiwa kuwa mateka, watatekwa mateka.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nao wakikuuliza, ‘Twende wapi?’ Waambie, ‘Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: “ ‘Wale waliowekwa kwa ajili ya kufa, na wafe; waliowekewa kufa kwa upanga, kwa upanga; waliowekewa kufa kwa njaa, kwa njaa; na waliowekewa kupelekwa uhamishoni, wapelekwe uhamishoni.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha itakuwa, hapo watakapokuambia, Tutoke, tuende wapi? Utawaambia, Bwana asema hivi, Walioandikiwa kufa, watakwenda kufa; au kufa kwa upanga, watakufa kwa upanga; au kufa kwa njaa, watakufa kwa njaa, au kutekwa nyara, watakuwa mateka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Na wakikuuliza, ‘Twende wapi?’ wewe utawajibu kuwa mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Waliopangiwa kufa kwa maradhi, watakufa kwa maradhi; waliopangiwa kufa kwa upanga, watakufa kwa upanga; waliopangiwa kufa kwa njaa, watakufa kwa njaa; na waliopangiwa kuwa mateka, watatekwa mateka.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nao kama wakikuuliza, ‘Tuende wapi?’ Waambie, ‘Hili ndilo BWANA asemalo: “ ‘Wale waliowekwa kwa ajili ya kufa, wakafe; waliowekwa kwa ajili ya upanga, kwa upanga; waliowekwa kwa ajili ya njaa, kwa njaa: waliowekwa kwa ajili ya kutekwa, watekwe.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nao kama wakikuuliza, ‘Twende wapi?’ Waambie, ‘Hili ndilo bwana asemalo: “ ‘Wale waliowekwa kwa ajili ya kufa, wakafe; waliowekwa kwa ajili ya upanga, kwa upanga; waliowekwa kwa ajili ya njaa, kwa njaa: waliowekwa kwa ajili ya kutekwa, watekwe.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha itakuwa, hapo watakapokuambia, Tutoke, tuende wapi? Utawaambia, BWANA asema hivi, Walioandikiwa kufa, watakwenda kufa; au kufa kwa upanga, watakufa kwa upanga; au kufa kwa njaa, watakufa kwa njaa, au kutekwa nyara, watakuwa mateka.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Na wakikuuliza, ‘Twende wapi?’ wewe utawajibu kuwa mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Waliopangiwa kufa kwa maradhi, watakufa kwa maradhi; waliopangiwa kufa kwa upanga, watakufa kwa upanga; waliopangiwa kufa kwa njaa, watakufa kwa njaa; na waliopangiwa kuwa mateka, watatekwa mateka.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kama wanakuuliza: Twende kwenda wapi? utawaambia: Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Kama ni kufa, nendeni kufa! Kama ni kuuawa na panga, nendeni kwenye panga! Kama ni kufa kwa njaa, nendeni kwenye njaa! Kama ni kutekwa, nendeni kutekwa!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha itakuwa, hapo watakapokuambia, Tutoke, tuende wapi? Utawaambia, BWANA asema hivi, Walioandikiwa kufa, watakwenda kufa; au kufa kwa upanga, watakufa kwa upanga; au kufa kwa njaa, watakufa kwa njaa, au kutekwa nyara, watakuwa mateka.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na kama wakikuuliza: Tutaenda wapi? Wewe utawajibu kwamba: Yawe anasema hivi: Walioandikiwa kufa kwa ugonjwa mukali, watakufa kwa ugonjwa mukali, walioandikiwa kufa kwa vita, watakufa kwa vita, walioandikwa kufa kwa njaa, watakufa kwa njaa; nao walioandikiwa kupelekwa katika utumwa, watapelekwa katika utumwa.