Jeremiah 15:3 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mimi Mwenyezi-Mungu nimeamua kuwaletea aina nne za maangamizi: Vita itakayowaua, mbwa watakaowararua; ndege wa angani watakaowadonoa na wanyama wa porini watakaowatafuna na kuwamaliza.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwenyezi Mungu asema, “Nitatuma aina nne za waangamizi: upanga ili kuua, mbwa ili kukokota mbali, ndege wa angani na wanyama wa nchi ili wale na waangamize.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nami nitaamrisha juu yao namna nne, asema Bwana; upanga uue, na mbwa wararue, na ndege wa angani, na wanyama wakali wa nchi, wale na kuangamiza.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mimi Mwenyezi-Mungu nimeamua kuwaletea aina nne za maangamizi: vita itakayowaua, mbwa watakaowararua; ndege wa angani watakaowadonoa na wanyama wa porini watakaowatafuna na kuwamaliza.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
BWANA asema, “Nitatuma aina nne ya waharabu dhidi yao, upanga ili kuua na mbwa ili wakokote mbali, ndege wa angani na wanyama wa nchi ili kula na kuangamiza.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bwana asema, “Nitatuma aina nne za waharabu dhidi yao: nazo ni upanga ili kuua na mbwa ili wakokote mbali, ndege wa angani na wanyama wa nchi ili kula na kuangamiza.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nami nitaamrisha juu yao namna nne, asema BWANA; upanga uue, na mbwa wararue, na ndege wa angani, na wanyama wakali wa nchi, wale na kuangamiza.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mimi Mwenyezi-Mungu nimeamua kuwaletea aina nne za maangamizi: Vita itakayowaua, mbwa watakaowararua; ndege wa angani watakaowadonoa na wanyama wa porini watakaowatafuna na kuwamaliza.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nitawapatia namna nne za mapatilizo; ndivyo, asemavyo Bwana: Panga za kuwaua, mbwa wa kuwakokotakokota, ndege wa angani na nyama wa porini wa kuwala na kuwamaliza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nami nitaamrisha juu yao namna nne, asema BWANA; upanga uue, na mbwa wararue, na ndege wa angani, na wanyama wakali wa nchi, wale na kuangamiza.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nimeamua kuleta aina ine za maangamizi juu yao: upanga kwa kuwaua, imbwa kwa kuwararua, ndege na nyama wa pori kwa kuwakula na kuwamaliza.