Jeremiah 15:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mama aliyesifika kuwa na watoto saba; sasa ghafla hana kitu. Ametoa pumzi yake ya mwisho, jua lake limetua kukiwa bado mchana; ameaibishwa na kufedheheshwa. Na wale waliobaki hai nitawaacha wauawe kwa upanga na maadui zao. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mama mwenye watoto saba atazimia na kupumua pumzi yake ya mwisho. Jua lake litatua kukiwa bado mchana, atatahayarika na kufedheheka. Wale wote waliobaki nitawaua kwa upanga mbele ya adui zao,” asema Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mwanamke aliyezaa watoto saba anazimia; ametoa roho; jua lake limekuchwa, ungali ni wakati wa mchana; ametahayarika na kufedheheka; na mabaki yao nitawatoa kwa upanga mbele ya adui zao, asema Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mama aliyesifika kuwa na watoto saba; sasa ghafla hana kitu. Ametoa pumzi yake ya mwisho, jua lake limetua kukiwa bado mchana; ameaibishwa na kufedheheshwa. Na wale waliobaki hai nitawaacha wauawe kwa upanga na maadui zao. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mama mwenye watoto saba atazimia na kupumua pumzi yake ya mwisho. Jua lake litatua kungali bado mchana, atatahayarika na kufedheheka. Wale wote waliobaki nitawaua kwa upanga mbele ya adui zao,” asema BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mama mwenye watoto saba atazimia na kupumua pumzi yake ya mwisho. Jua lake litatua kungali bado mchana, atatahayarika na kufedheheka. Wale wote waliobaki nitawaua kwa upanga mbele ya adui zao,” asema bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mwanamke aliyezaa watoto saba anazimia; ametoa roho; jua lake limekuchwa, ikiwa bado ni wakati wa mchana; ameaibika na kutwezwa; na mabaki yao nitawatoa kwa upanga mbele ya adui zao, asema BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mama aliyesifika kuwa na watoto saba; sasa ghafla hana kitu. Ametoa pumzi yake ya mwisho, jua lake limetua kukiwa bado mchana; ameaibishwa na kufedheheshwa. Na wale waliobaki hai nitawaacha wauawe kwa upanga na maadui zao. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Aliyezaa wana saba akazimia kwa uchungu, akakatika roho yake, kwa kuona soni na kujifunika jua lake likachwa, mchana ungaliko bado. Nayo masao yao nitayatoa, wauawe na panga za adui zao; ndivyo, asemavyo Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mwanamke aliyezaa watoto saba anazimia; ametoa roho; jua lake limekuchwa, ungali ni wakati wa mchana; ametahayarika na kufedheheka; na mabaki yao nitawatoa kwa upanga mbele ya adui zao, asema BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mama aliyeheshimiwa kwa kuwa na watoto saba, sasa kwa rafla hana kitu. Amezimia na kukata roho, amekufa angali kijana, amefezeheka na kuzarauliwa. Na wale watakaobaki wazima nitawatoa kwa upanga mbele ya waadui zao. –Ni ujumbe wa Yawe.