Jeremiah 16:15 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
bali wataapa kwa kusema, ‘Kama aishivyo Mwenyezi-Mungu aliyewatoa Waisraeli kutoka nchi ya kaskazini na kutoka katika nchi zote alikowafukuzia!’ Maana, nitawarudisha katika nchi yao niliyowapa wazee wao.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
bali watasema, ‘Hakika kama Mwenyezi Mungu aishivyo, aliyewatoa Waisraeli kutoka nchi ya kaskazini na nchi zote alizokuwa amewafukuzia.’ Maana nitawarudisha katika nchi niliyowapa baba zao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
lakini, Aishivyo Bwana, aliyewaleta wana wa Israeli toka nchi ya kaskazini, na toka nchi zote alikowafukuza; nami nitawarudisha katika nchi yao wenyewe niliyowapa baba zao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
bali wataapa kwa kusema, ‘Kama aishivyo Mwenyezi-Mungu aliyewatoa Waisraeli kutoka nchi ya kaskazini na kutoka katika nchi zote alikowafukuzia!’ Maana, nitawarudisha katika nchi yao niliyowapa wazee wao.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
bali watasema, ‘Hakika kama BWANA aishivyo, aliyewatoa wana wa Israeli kutoka katika nchi ya kaskazini na nchi zote ambako alikuwa amewafukuzia.’ Maana nitawarudisha katika nchi niliyowapa baba zao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bali watasema, ‘Hakika kama bwana aishivyo, aliyewatoa wana wa Israeli kutoka nchi ya kaskazini na nchi zote alizokuwa amewafukuzia.’ Maana nitawarudisha katika nchi niliyowapa baba zao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
lakini, Aishivyo BWANA, aliyewaleta wana wa Israeli toka nchi ya kaskazini, na toka nchi zote alikowafukuza; nami nitawarudisha katika nchi yao wenyewe niliyowapa baba zao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
bali wataapa kwa kusema, ‘Kama aishivyo Mwenyezi-Mungu aliyewatoa Waisraeli kutoka nchi ya kaskazini na kutoka katika nchi zote alikowafukuzia!’ Maana, nitawarudisha katika nchi yao niliyowapa wazee wao.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ila wataapa wakisema: Hivyo, Bwana alivyo Mwenye uzima aliyewatoa wana wa Isiraeli katika nchi ya upande wa kaskazini na katika nchi zote, alikowatupia! Maana nitawarudisha katika nchi yao, niliyowapa baba zao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
lakini, Aishivyo BWANA, aliyewaleta wana wa Israeli toka nchi ya kaskazini, na toka nchi zote alikowafukuza; nami nitawarudisha katika nchi yao wenyewe niliyowapa baba zao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini wataapa wakisema: Kama vile Yawe anavyoishi, yule aliyewaondoa Waisraeli kutoka katika inchi ya kaskazini na kutoka katika inchi zote ambapo alipowasambaza. Maana, nitawarudisha katika inchi yao niliyowapatia babu zao. –Ni ujumbe wa Yawe.