Jeremiah 16:19 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ee Mwenyezi-Mungu! Wewe ndiwe nguvu yangu na ngome yangu; wewe ni kimbilio langu wakati wa taabu. Mataifa toka pande zote duniani yatakujia na kusema: “Wazee wetu hawakuwa na kitu ila miungu ya uongo, vitu duni visivyo na faida yoyote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ee Mwenyezi Mungu, nguvu zangu na ngome yangu, kimbilio langu wakati wa taabu, kwako mataifa watakujia kutoka miisho ya dunia na kusema, “Baba zetu hawakuwa na chochote isipokuwa miungu ya uongo, sanamu batili ambazo hazikuwafaidi kitu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ee Bwana, nguvu zangu, ngome yangu, na kimbilio langu siku ya taabu, kwako wewe watakuja mataifa yote toka ncha za dunia, wakisema, Baba zenu hawakurithi kitu ila uongo, naam, ubatili na vitu visivyofaa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ee Mwenyezi-Mungu! Wewe ndiwe nguvu yangu na ngome yangu; wewe ni kimbilio langu wakati wa taabu. Mataifa toka pande zote duniani yatakujia na kusema: “Wazee wetu hawakuwa na kitu ila miungu ya uongo, vitu duni visivyo na faida yoyote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ee BWANA, nguvu zangu na ngome yangu, kimbilio langu wakati wa taabu, kwako mataifa yatakujia kutoka miisho ya dunia na kusema, “Baba zetu hawakuwa na cho chote zaidi ya miungu ya uongo, sanamu zisizofaa kitu ambazo hazikuwafaidia lo lote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ee bwana, nguvu zangu na ngome yangu, kimbilio langu wakati wa taabu, kwako mataifa yatakujia kutoka miisho ya dunia na kusema, “Baba zetu hawakuwa na chochote zaidi ya miungu ya uongo, sanamu zisizofaa kitu ambazo hazikuwafaidia lolote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ee BWANA, nguvu zangu, ngome yangu, na kimbilio langu siku ya taabu, kwako wewe watakuja mataifa yote toka ncha za dunia, wakisema, Baba zenu hawakurithi kitu ila uongo, naam, ubatili na vitu visivyofaa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ee Mwenyezi-Mungu! Wewe ndiwe nguvu yangu na ngome yangu; wewe ni kimbilio langu wakati wa taabu. Mataifa toka pande zote duniani yatakujia na kusema: “Wazee wetu hawakuwa na kitu ila miungu ya uongo, vitu duni visivyo na faida yoyote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana ndiwe nguvu yangu na ngome yangu na kimbilio langu siku ya masongano; wewe watakujia wamizimu wakitoka mapeoni kwa nchi, watakuambia: Baba zetu waliyokuwa nayo, ni mambo ya uwongo tu yasiyo maana, yasiyowafalia kitu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ee BWANA, nguvu zangu, ngome yangu, na kimbilio langu siku ya taabu, kwako wewe watakuja mataifa yote toka ncha za dunia, wakisema, Baba zenu hawakurithi kitu ila uongo, naam, ubatili na vitu visivyofaa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ee Yawe! Wewe ndiwe nguvu yangu na upango wangu; wewe ni kimbilio langu wakati wa taabu. Mataifa toka pande zote za dunia yatakufikia na kusema: Miungu ya babu zetu ilikuwa ya uongo, ilikuwa ya bure, isiyofaa kitu.