Jeremiah 16:3 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi juu ya watoto wa kiume na wa kike watakaozaliwa mahali hapa, na juu ya wazazi wao:
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu kuhusu wana wa kiume na wa kike wanaozaliwa katika nchi hii, na kuhusu wale wanawake ambao ni mama zao, na wale wanaume ambao ni baba zao:
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana Bwana asema hivi, katika habari za wana, na katika habari za binti, wazaliwao mahali hapa, na katika habari za mama zao waliowazaa, na katika habari za baba zao waliowazaa, katika nchi hii;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi juu ya watoto wa kiume na wa kike watakaozaliwa mahali hapa, na juu ya wazazi wao:
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana hilo ndilo asemalo BWANA kuhusu wana na binti wazaliwao katika nchi hii na kuhusu wale wanawake ambao ni mama zao na wale wanaume ambao ni baba zao:
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana hili ndilo asemalo bwana kuhusu wana na binti wazaliwao katika nchi hii, na kuhusu wale wanawake ambao ni mama zao, na wale wanaume ambao ni baba zao:
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana BWANA asema hivi, kuhusu habari za wana, na kuhusu habari za binti, wazaliwao mahali hapa, na kuhusu habari za mama zao waliowazaa, na kuhusu habari za baba zao waliowazaa, katika nchi hii;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi juu ya watoto wa kiume na wa kike watakaozaliwa mahali hapa, na juu ya wazazi wao:
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani hivi ndivyo, Bwana anavyosema kwa ajili ya wana wa kiume na wa kike wanaozaliwa mahali hapa na kwa ajili ya mama zao waliowazaa na kwa ajili ya baba zao waliowazaa katika nchi hii:
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana BWANA asema hivi, katika habari za wana, na katika habari za binti, wazaliwao mahali hapa, na katika habari za mama zao waliowazaa, na katika habari za baba zao waliowazaa, katika nchi hii;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Maana Yawe anasema hivi juu ya wana na wabinti watakaozaliwa pahali hapa na juu ya wazazi wao: