Jeremiah 16:4 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hao watakufa kwa maradhi mabaya, na hakuna atakayewaombolezea wala kuwazika. Maiti zao zitazagaa kama mavi juu ya ardhi. Wataangamia kwa upanga na kwa njaa; na maiti zao zitakuwa chakula cha ndege wa angani na wanyama wakali wa nchi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Watakufa kwa magonjwa ya kufisha. Hawataombolezewa wala kuzikwa, lakini watakuwa kama kinyesi juu ya ardhi. Watakufa kwa upanga na kwa njaa. Mizoga yao itakuwa chakula cha ndege na wanyama wa porini.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
watakufa kwa maradhi mabaya; hawataliliwa, wala hawatazikwa; watakuwa kama samadi juu ya uso wa nchi; nao wataangamizwa kwa upanga, na kwa njaa; na mizoga yao itakuwa chakula cha ndege wa angani, na cha wanyama wa nchi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hao watakufa kwa maradhi mabaya, na hakuna atakayewaombolezea wala kuwazika. Maiti zao zitazagaa kama mavi juu ya ardhi. Wataangamia kwa upanga na kwa njaa; na maiti zao zitakuwa chakula cha ndege wa angani na wanyama wakali wa nchi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Watakufa kwa magonjwa ya kufisha. Hawataombolezewa wala kuzikwa lakini watakuwa kama mavi yaliyosambaa juu ya ardhi. Watakufa kwa upanga na kwa njaa, nazo maiti zao zitakuwa chakula cha ndege wa angani na cha wanyama wa nchi.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Watakufa kwa magonjwa ya kufisha. Hawataombolezewa wala kuzikwa, lakini watakuwa kama mavi yaliyosambaa juu ya ardhi. Watakufa kwa upanga na kwa njaa, nazo maiti zao zitakuwa chakula cha ndege wa angani, na cha wanyama wa nchi.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
watakufa kwa maradhi mabaya; hawataliliwa, wala hawatazikwa; watakuwa kama samadi juu ya uso wa nchi; nao wataangamizwa kwa upanga, na kwa njaa; na mizoga yao itakuwa chakula cha ndege wa angani, na cha wanyama wa nchi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hao watakufa kwa maradhi mabaya, na hakuna atakayewaombolezea wala kuwazika. Maiti zao zitazagaa kama mavi juu ya ardhi. Wataangamia kwa upanga na kwa njaa; na maiti zao zitakuwa chakula cha ndege wa angani na wanyama wakali wa nchi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Watakufa kwa magonjwa mabaya, hawataombolezewa, wala hawatazikwa, ila watakuwa tu kama kinyesi juu ya nchi; wengine watauawa kwa panga na kwa njaa, nayo mizoga yao itakuwa chakula cha ndege wa angani na cha nyama wa porini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
watakufa kwa maradhi mabaya; hawataliliwa, wala hawatazikwa; watakuwa kama samadi juu ya uso wa nchi; nao wataangamizwa kwa upanga, na kwa njaa; na mizoga yao itakuwa chakula cha ndege wa angani, na cha wanyama wa nchi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hao watakufa kwa magonjwa makali, na hakuna atakayeomboleza juu yao wala kuwazika. Maiti zao zitabaki kama vile mboleo juu ya udongo. Wataangamia kwa vita na kwa njaa; na maiti zao zitakuwa chakula cha ndege na nyama wa pori.