Jeremiah 16:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Maana mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Usiingie kabisa katika nyumba ya matanga wala usiende kuomboleza wala kuwalilia. Kwa maana nimeondoa amani yangu, fadhili zangu na huruma yangu kutoka kwa watu hawa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa kuwa hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: “Usiingie katika nyumba ambayo kuna chakula cha matanga; usiende kuwaombolezea wala kuwahurumia, kwa sababu nimeondoa amani yangu, upendo wangu na huruma zangu kutoka kwa watu hawa,” asema Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana Bwana asema hivi, Usiingie ndani ya nyumba yenye matanga, wala usiende kuwaombolezea, wala kuwalilia; maana nimewaondolea watu hawa amani yangu, asema Bwana, hata fadhili zangu na rehema zangu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Maana mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Usiingie kabisa katika nyumba ya matanga wala usiende kuomboleza wala kuwalilia. Kwa maana nimeondoa amani yangu, fadhili zangu na huruma yangu kutoka kwa watu hawa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa kuwa hili ndilo asemalo BWANA: “Usiingie katika nyumba ambayo kuna chakula cha matanga, usiende kuwaombolezea wala kuwahurumia, kwa sababu nimeziondoa baraka zangu, upendo wangu na huruma zangu kutoka kwa watu hawa,” asema BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa kuwa hili ndilo asemalo bwana: “Usiingie katika nyumba ambayo kuna chakula cha matanga, usiende kuwaombolezea wala kuwahurumia, kwa sababu nimeziondoa baraka zangu, upendo wangu na huruma zangu kutoka kwa watu hawa,” asema bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana BWANA asema hivi, Usiingie ndani ya nyumba yenye matanga, wala usiende kuwaombolezea, wala kuwalilia; maana nimewaondolea watu hawa amani yangu, asema BWANA, hata fadhili zangu na rehema zangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Maana mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Usiingie kabisa katika nyumba ya matanga wala usiende kuomboleza wala kuwalilia. Kwa maana nimeondoa amani yangu, fadhili zangu na huruma yangu kutoka kwa watu hawa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Usiingie nyumbani mwenye maombolezo, wala usiende kuwalilia, wala usiwakalie matanga! Kwani nimeuondoa utengemano wangu kwao walio ukoo huu, nisiwagawie chema, wala nisiwahurumie; ndivyo, asemavyo Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana BWANA asema hivi, Usiingie ndani ya nyumba yenye matanga, wala usiende kuwaombolezea, wala kuwalilia; maana nimewaondolea watu hawa amani yangu, asema BWANA, hata fadhili zangu na rehema zangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe anasema hivi: Usiingie katika nyumba yenye kilio wala usiende kuomboleza wala kuwalilia. Kwa maana sitawapatia watu hawa amani tena. Sitawatendea tena mema wala kuwasikilia huruma. –Ni ujumbe wa Yawe.–