Jeremiah 16:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wote, wakubwa kwa wadogo, watakufa katika nchi hii; nao hawatazikwa, wala hakuna atakayewaombolezea. Hakuna atakayejikatakata au kunyoa upara wa matanga.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Wakubwa na wadogo watakufa katika nchi hii. Hawatazikwa wala kuombolezewa, na hakuna atakayejikatakata au kunyoa nywele za kichwa chake kwa ajili yao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakubwa kwa wadogo wote pia watakufa katika nchi hii; hawatazikwa, wala watu hawatawalilia, wala kujikata-kata kwa ajili yao, wala kujinyoa kwa ajili yao;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wote, wakubwa kwa wadogo, watakufa katika nchi hii; nao hawatazikwa, wala hakuna atakayewaombolezea. Hakuna atakayejikatakata au kunyoa upara wa matanga.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Wakubwa na wadogo watakufa katika nchi hii. Hawatazikwa wala kuombolezewa, hakuna atakayejikatakata au kunyoa nywele za kichwa chake kwa ajili yao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Wakubwa na wadogo watakufa katika nchi hii. Hawatazikwa wala kuombolezewa, na hakuna atakayejikatakata au kunyoa nywele za kichwa chake kwa ajili yao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakubwa kwa wadogo wote pia watakufa katika nchi hii; hawatazikwa, wala watu hawatawalilia, wala kujikatakata kwa ajili yao, wala kujinyoa kwa ajili yao;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wote, wakubwa kwa wadogo, watakufa katika nchi hii; nao hawatazikwa, wala hakuna atakayewaombolezea. Hakuna atakayejikatakata au kunyoa upara wa matanga.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Watakufa wakubwa na wadogo katika nchi hii pasipo kuzikwa, tena hakuna watakaowalilia wala watakaojikata chale wala watakaonyoa vichwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakubwa kwa wadogo wote pia watakufa katika nchi hii; hawatazikwa, wala watu hawatawalilia, wala kujikata-kata kwa ajili yao, wala kujinyoa kwa ajili yao;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wote, wakubwa kama vile wadogo, watakufa katika inchi hii; nao hawatazikwa, wala hakuna atakayeomboleza juu yao. Hakuna atakayejikatakata wala kunyolewa upaa kwa ajili ya kifo chao.