Jeremiah 17:11 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mtu apataye mali isiyo halali ni kama kware akusanyaye makinda ambayo hakuyaangua: Wakati wa kilele cha ujana wake itamchopoka, na mwishoni atakuwa mtu mpumbavu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kama kware aanguaye mayai asiyoyataga, ndivyo alivyo mtu apataye mali kwa njia zisizo za haki. Maisha yake yatakapofika katikati, siku zitamwacha, na mwishoni atabainika kuwa mpumbavu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kama kware akusanyaye makinda asiyoyazaa, ndivyo alivyo mtu ajipatiaye mali, wala si kwa haki, katikati ya siku zake zitaachana naye, na mwisho wake atakuwa mpumbavu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mtu apataye mali isiyo halali ni kama kware akusanyaye makinda ambayo hakuyaangua: wakati wa kilele cha ujana wake itamchopoka, na mwishoni atakuwa mtu mpumbavu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama kware aanguaye mayai asiyoyataga, ndivyo alivyo mtu apataye mali kwa njia zisizo za haki. Maisha yake yafikapo katikati, siku zitamwacha, na mwishoni atabainika kuwa mpumbavu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama kware aanguaye mayai asiyoyataga, ndivyo alivyo mtu apataye mali kwa njia zisizo za haki. Maisha yake yafikapo katikati, siku zitamwacha, na mwishoni atabainika kuwa mpumbavu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kama kware akusanyaye makinda asiyoyaangua, ndivyo alivyo mtu ajipatiaye mali, wala si kwa haki, katikati ya maisha yake itamtoka, na mwisho wake atakuwa mpumbavu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mtu apataye mali isiyo halali ni kama kware akusanyaye makinda ambayo hakuyaangua: Wakati wa kilele cha ujana wake itamchopoka, na mwishoni atakuwa mtu mpumbavu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kama kwale anayelalia mayai, asiyoyataga, ndivyo, alivyo apataye mali kwa kupotoa watu; siku zake zitakapofika kati, zitampotelea, naye mwisho atapumbaa tu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kama kware akusanyaye makinda asiyoyazaa, ndivyo alivyo mtu ajipatiaye mali, wala si kwa haki, katikati ya siku zake zitaachana naye, na mwisho wake atakuwa mpumbavu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutu anayepata mali isiyokuwa ya usawa ni kama kwale anayelalia mayai ambayo hakutaga. Mali yanamwishia angali kijana, na kwa mwisho anageuka sawa mupumbafu.