Jeremiah 17:18 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Waaibishwe wale wanaonitesa, lakini mimi usiniache niaibike. Wafedheheshwe watu hao, lakini mimi usiniache nifedheheke. Uwaletee siku ya maafa, waangamize kwa maangamizi maradufu!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watesi wangu na waaibishwe, lakini nilinde mimi nisiaibike; wao na watiwe hofu kuu, lakini unilinde mimi na hofu kuu. Waletee siku ya maafa; waangamize kwa maangamizi maradufu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na waaibike watu wanaoniudhi, lakini nisiaibike mimi; na waone hofu kuu, lakini mimi nisione hofu kuu; ulete juu yao siku ya uovu; uwaangamize maangamizo maradufu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Waaibishwe wale wanaonitesa, lakini mimi usiniache niaibike. Wafedheheshwe watu hao, lakini mimi usiniache nifedheheke. Uwaletee siku ya maafa, waangamize kwa maangamizi maradufu!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Watesi wangu na waaibishwe, lakini nilinde mimi nisiaibike; wao na watiwe hofu kuu, lakini unilinde mimi na hofu kuu. Uwaletee siku ya maafa; waangamize kwa maangamizi maradufu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watesi wangu na waaibishwe, lakini nilinde mimi nisiaibike; wao na watiwe hofu kuu, lakini unilinde mimi na hofu kuu. Waletee siku ya maafa; waangamize kwa maangamizi maradufu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na waaibike watu wanaoniudhi, lakini nisiaibike mimi; na waone hofu kuu, lakini mimi nisione hofu kuu; ulete juu yao siku ya uovu; uwaangamize maangamizo maradufu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Waaibishwe wale wanaonitesa, lakini mimi usiniache niaibike. Wafedheheshwe watu hao, lakini mimi usiniache nifedheheke. Uwaletee siku ya maafa, waangamize kwa maangamizi maradufu!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Na wapatwe na soni wanikimbizao, nisipatwe na soni mimi! Na waangamie wao, nisiangamie mimi! Uwaletee wao siku mbaya! Mara mbili uwavunje, wavunjike kweli!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na waaibike watu wanaoniudhi, lakini nisiaibike mimi; na waone hofu kuu, lakini mimi nisione hofu kuu; ulete juu yao siku ya uovu; uwaangamize maangamizo maradufu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Uwapatishe haya wale wanaonitesa, lakini usiniache mimi kupata haya. Uwafezeheshe watu hao, lakini usiniache mimi kufezeheka. Uwaletee ile siku ya hasara, uwaangamize kabisakabisa!