Jeremiah 17:19 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu aliniambia hivi: “Nenda ukasimame penye lango la watu ambapo wafalme wa Yuda huingia na kutoka mjini, na katika malango mengine yote ya Yerusalemu useme:
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hili ndilo Mwenyezi Mungu aliloniambia: “Nenda ukasimame kwenye lango la watu, mahali ambako wafalme wa Yuda huingilia na kutokea; simama pia kwenye malango mengine yote ya Yerusalemu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana akaniambia hivi, Enenda ukasimame katika lango la wana wa watu hawa, waingiapo wafalme wa Yuda, na watokeapo, na katika malango yote ya Yerusalemu,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu aliniambia hivi: “Nenda ukasimame penye lango la watu ambapo wafalme wa Yuda huingia na kutoka mjini, na katika malango mengine yote ya Yerusalemu useme:
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hili ndilo BWANA aliloniambia: “Nenda ukasimame kwenye lango la watu, mahali ambako wafalme wa Yuda huingilia na kutokea, simama pia kwenye malango mengine yote ya Yerusalemu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hili ndilo bwana aliloniambia: “Nenda ukasimame kwenye lango la watu, mahali ambako wafalme wa Yuda huingilia na kutokea, simama pia kwenye malango mengine yote ya Yerusalemu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA akaniambia hivi, Nenda ukasimame katika lango la wana wa watu hawa, waingiapo wafalme wa Yuda, na watokeapo, na katika malango yote ya Yerusalemu,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu aliniambia hivi: “Nenda ukasimame penye lango la watu ambapo wafalme wa Yuda huingia na kutoka mjini, na katika malango mengine yote ya Yerusalemu useme:
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivi ndivyo, Bwana alivyoniambia: Nenda kusimama langoni mwao walio wazaliwa wa ukoo huu, wafalme wa Yuda walimopitia wakiingia au wakitoka, hata malangoni mote mwa Yerusalemu,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA akaniambia hivi, Enenda ukasimame katika lango la wana wa watu hawa, waingiapo wafalme wa Yuda, na watokeapo, na katika malango yote ya Yerusalemu,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe aliniambia hivi: Kwenda usimame kwenye Mulango wa Wanainchi, ambako wafalme wa Yuda wanapitia wanapoingia au kutoka Yerusalema. Uende vilevile kwenye milango yake yote ingine na kutangaza hivi: