Jeremiah 17:24 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Lakini mkinisikiliza mimi Mwenyezi-Mungu, mkaacha kuingiza mzigo wowote kupitia malango ya mji huu siku ya Sabato, wala kufanya kazi siku hiyo,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini mkiwa waangalifu kunitii, asema Mwenyezi Mungu, nanyi msipoleta mzigo wowote kupitia malango ya mji huu wakati wa Sabato, lakini mkaitakasa siku ya Sabato kwa kutofanya kazi siku hiyo,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na itakuwa, kama mkinisikiliza mimi kwa bidii, asema Bwana, msiingize mzigo wo wote kwa malango ya mji huu siku ya sabato, bali mkiitakasa siku ya sabato, bila kufanya kazi yo yote siku hiyo;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Lakini mkinisikiliza mimi Mwenyezi-Mungu, mkaacha kuingiza mzigo wowote kupitia malango ya mji huu siku ya Sabato, wala kufanya kazi siku hiyo,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini mkiwa waangalifu katika kunitii, asema BWANA, nanyi msipoleta mzigo wo wote kupitia malango ya mji huu wakati wa Sabato, lakini mkaitakasa siku ya Sabato kwa kutofanya kazi siku hiyo,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini mkiwa waangalifu kunitii, asema bwana, nanyi msipoleta mzigo wowote kupitia malango ya mji huu wakati wa Sabato, lakini mkaitakasa siku ya Sabato kwa kutofanya kazi siku hiyo,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na itakuwa, kama mkinisikiliza mimi kwa bidii, asema BWANA, msiingize mzigo wowote katika mlango wa mji huu siku ya sabato, bali muitakase siku ya sabato, bila kufanya kazi yoyote siku hiyo;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Lakini mkinisikiliza mimi Mwenyezi-Mungu, mkaacha kuingiza mzigo wowote kupitia malango ya mji huu siku ya Sabato, wala kufanya kazi siku hiyo,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndivyo, asemavyo Bwana: Sasa ninyi nisikieni, msiingize mzigo malangoni mwa mji huu siku ya mapumziko! Ila itakaseni siku ya mapumziko, msipoifanyizia kazi yo yote!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na itakuwa, kama mkinisikiliza mimi kwa bidii, asema BWANA, msiingize mzigo wo wote kwa malango ya mji huu siku ya sabato, bali mkiitakasa siku ya sabato, bila kufanya kazi yo yote siku hiyo;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini ninyi munisikilize mimi. Muache kuingiza muzigo wowote kupitia kwenye milango ya muji huu siku ya Sabato, muihesabu kuwa takatifu na kutofanya kazi.