Jeremiah 17:25 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
basi, wafalme na wana wa wafalme wanaomfuata mfalme Daudi katika utawala, pamoja na watu wa Yuda na wakazi wa Yerusalemu, wataingia kwa kupitia malango ya mji huu, wakiwa wamepanda farasi na magari ya farasi. Nao mji huu utakuwa na watu daima.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
ndipo wafalme wanaokaa kwenye kiti cha utawala cha Daudi wataingia kupitia malango ya mji huu, pamoja na maafisa wao. Wafalme na maafisa wao watakuja wakiwa wamepanda magari ya vita na farasi, wakiandamana na watu wote wa Yuda na wakaaji wa Yerusalemu, nao mji huu utakaliwa na watu daima.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ndipo watakapoingia wafalme na wakuu kwa malango ya mji huu; wataketi katika kiti cha enzi cha Daudi, na kupanda magari na farasi, wao, na wakuu wao, watu wa Yuda, na wenyeji wa Yerusalemu; na mji huu utakaa hata milele.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
basi, wafalme na wana wa wafalme wanaomfuata mfalme Daudi katika utawala, pamoja na watu wa Yuda na wakazi wa Yerusalemu, wataingia kwa kupitia malango ya mji huu, wakiwa wamepanda farasi na magari ya farasi. Nao mji huu utakuwa na watu daima.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
ndipo wafalme wakaao juu ya kiti cha enzi cha Daudi, wataingia kupitia malango ya mji huu pamoja na maafisa wao. Wao na maafisa wao watakuja wakiwa wamepanda magari na farasi, wakiandamana na watu wa Yuda na wale waishio Yerusalemu, nao mji huu utakaliwa na watu daima.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
ndipo wafalme wakaao juu ya kiti cha enzi cha Daudi wataingia kupitia malango ya mji huu, pamoja na maafisa wao. Wao na maafisa wao watakuja wakiwa wamepanda magari na farasi, wakiandamana na watu wa Yuda na wale waishio Yerusalemu, nao mji huu utakaliwa na watu daima.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ndipo watakapoingia wafalme na wakuu kwa malango ya mji huu; wataketi katika kiti cha enzi cha Daudi, na kupanda magari na farasi, wao, na wakuu wao, watu wa Yuda, na wenyeji wa Yerusalemu; na mji huu utakaa hata milele.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
basi, wafalme na wana wa wafalme wanaomfuata mfalme Daudi katika utawala, pamoja na watu wa Yuda na wakazi wa Yerusalemu, wataingia kwa kupitia malango ya mji huu, wakiwa wamepanda farasi na magari ya farasi. Nao mji huu utakuwa na watu daima.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, watakapoingia humu malangoni mwa mji huu wafalme wanaokikalia kiti cha kifalme cha Dawidi na wakuu wanaopanda magari na farasi, wao wenyewe na wakuu wao, Wayuda nao wakaao Yerusalemu, nao mji huu utakaa kale na kale.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ndipo watakapoingia wafalme na wakuu kwa malango ya mji huu; wataketi katika kiti cha enzi cha Daudi, na kupanda magari na farasi, wao, na wakuu wao, watu wa Yuda, na wenyeji wa Yerusalemu; na mji huu utakaa hata milele.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu, wafalme na wana wao watakaotawala nyuma juu ya kiti cha kifalme cha Daudi, wanaopanda juu ya farasi na magari yenye kukokotwa pamoja na watu wa Yuda na wakaaji wa Yerusalema, wataendelea kuingia ndani ya muji huu wakipitia kwenye milango hii. Nao muji huu utaikaliwa na watu siku zote.