Jeremiah 17:26 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu watakuja kutoka miji ya Yuda na maeneo ya kandokando ya Yerusalemu, kutoka nchi ya Benyamini, kutoka Shefela, kutoka nchi ya milima na kutoka Negebu, wakileta sadaka za kuteketezwa na tambiko, sadaka za nafaka na ubani wa harufu nzuri, pamoja na matoleo ya shukrani. Vyote hivyo watavileta katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watu watakuja kutoka miji ya Yuda na vijiji vinavyoizunguka Yerusalemu, kutoka nchi ya Benyamini na Shefela, kutoka nchi ya vilima na Negebu, wakileta sadaka za kuteketezwa na dhabihu, sadaka za nafaka, uvumba na sadaka za shukrani kwenye nyumba ya Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao watatoka miji ya Yuda, na mahali palipo pande zote za Yerusalemu, na nchi ya Benyamini, na Shefela,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu watakuja kutoka miji ya Yuda na maeneo ya kandokando ya Yerusalemu, kutoka nchi ya Benyamini, kutoka Shefela, kutoka nchi ya milima na kutoka Negebu, wakileta sadaka za kuteketezwa na tambiko, sadaka za nafaka na ubani wa harufu nzuri, pamoja na matoleo ya shukrani. Vyote hivyo watavileta katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Watu watakuja kutoka miji ya Yuda na vijiji vinavyoizunguka Yerusalemu, kutoka nchi ya Benyamini na chini ya vilima vya magharibi, kutoka nchi ya vilima na Negebu, wakileta sadaka za kuteketezwa na dhabihu, sadaka za nafaka, uvumba na sadaka za shukrani kwenye nyumba ya BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watu watakuja kutoka miji ya Yuda na vijiji vinavyoizunguka Yerusalemu, kutoka nchi ya Benyamini na chini ya vilima vya magharibi, kutoka nchi ya vilima na Negebu, wakileta sadaka za kuteketezwa na dhabihu, sadaka za nafaka, uvumba na sadaka za shukrani kwenye nyumba ya bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao watatoka miji ya Yuda, na mahali palipo pande zote za Yerusalemu, na nchi ya Benyamini, na Shefela, na milima, na upande wa Negebu, wakileta sadaka za kuteketezwa, na dhabihu, na sadaka za unga, na ubani, wakileta pia sadaka za shukrani, nyumbani kwa BWANA
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu watakuja kutoka miji ya Yuda na maeneo ya kandokando ya Yerusalemu, kutoka nchi ya Benyamini, kutoka Shefela, kutoka nchi ya milima na kutoka Negebu, wakileta sadaka za kuteketezwa na tambiko, sadaka za nafaka na ubani wa harufu nzuri, pamoja na matoleo ya shukrani. Vyote hivyo watavileta katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena watakuja wakitoka katika miji ya Yuda na katika nchi zizungukazo Yerusalemu na katika nchi ya Benyamini, kwenye mbuga na kwenye milima, hata upande wa kusini, wataleta ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima na za kuchinjwa na vipaji vingine vya tambiko na uvumba, wataviingiza Nyumbani mwa Bwana, wamshukuru.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao watatoka miji ya Yuda, na mahali palipo pande zote za Yerusalemu, na nchi ya Benyamini, na Shefela, na milima, na upande wa Negebu, wakileta sadaka za kuteketezwa, na dhabihu, na sadaka za unga, na ubani, wakileta pia sadaka za shukrani, nyumbani kwa BWANA
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu watakuja kutoka miji ya Yuda na maeneo ya kandokando ya Yerusalema, kutoka inchi ya kabila la Benjamina, kutoka Shefela, kutoka inchi ya milima na kutoka Negebu, wakileta sadaka za kuteketezwa kwa moto na sadaka zingine za kawaida, sadaka ya mavuno na ya ubani wenye harufu nzuri pamoja na matoleo ya shukrani. Hivyo vyote watavileta katika nyumba ya Yawe.