Jeremiah 18:15 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini watu wangu wamenisahau mimi, wanafukizia ubani miungu ya uongo. Wamejikwaa katika njia zao, katika barabara za zamani. Wanapitia vichochoroni badala ya njia kuu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini watu wangu wamenisahau mimi, wanafukizia uvumba sanamu batili, zilizowafanya wajikwae katika njia zao na katika mapito ya zamani. Zimewafanya wapite kwenye vichochoro na kwenye barabara ambazo hazikujengwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana watu wangu wamenisahau, wameufukizia ubatili uvumba; nao wamewakaza katika njia zao, katika mapito ya zamani, ili wapite katika njia za kando, katika njia isiyotengenezwa;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini watu wangu wamenisahau mimi, wanafukizia ubani miungu ya uongo. Wamejikwaa katika njia zao, katika barabara za zamani. Wanapitia vichochoroni badala ya njia kuu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini watu wangu wamenisahau mimi, wanafukizia uvumba sanamu zisizofaa kitu, zilizowafanya wajikwae katika njia zao na katika mapito ya zamani. Zimewafanya wapite kwenye vichochoro na kwenye barabara ambazo hazikujengwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini watu wangu wamenisahau mimi, wanafukizia uvumba sanamu zisizofaa kitu, zilizowafanya wajikwae katika njia zao na katika mapito ya zamani. Zimewafanya wapite kwenye vichochoro na kwenye barabara ambazo hazikujengwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana watu wangu wamenisahau, wameufukizia ubatili uvumba; nao wamewakaza katika njia zao, katika mapito ya zamani, ili wapite katika njia za kando, katika njia isiyotengenezwa;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini watu wangu wamenisahau mimi, wanafukizia ubani miungu ya uongo. Wamejikwaa katika njia zao, katika barabara za zamani. Wanapitia vichochoroni badala ya njia kuu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini walio ukoo wangu wamenisahau, huvukizia miungu isiyo kitu, nayo ikawaangusha katika njia zao, walizozishika tangu kale, wakafuata mikondo isiyotengenezwa kuwa njia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana watu wangu wamenisahau, wameufukizia ubatili uvumba; nao wamewakaza katika njia zao, katika mapito ya zamani, ili wapite katika njia za kando, katika njia isiyotengenezwa;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini watu wangu wamenisahau mimi, wanaifukizia miungu ya uongo ubani. Wamejikwaa katika njia zao, wameacha barabara zao za zamani.