Jeremiah 18:6 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Enyi Waisraeli! Je, mimi Mwenyezi-Mungu siwezi kuwafanya nyinyi kama alivyofanya mfinyanzi huyu? Jueni kuwa kama ulivyo udongo mikononi mwa mfinyanzi, ndivyo nyinyi mlivyo mikononi mwangu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Ee nyumba ya Israeli, je, siwezi kuwafanyia kama huyu mfinyanzi afanyavyo?” asema Mwenyezi Mungu. “Kama vile udongo ulivyo katika mikono ya mfinyanzi, ndivyo mlivyo katika mkono wangu, ee nyumba ya Israeli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ee nyumba ya Israeli, je! Siwezi mimi kuwatendea ninyi vile vile kama mfinyanzi huyu alivyotenda? Asema Bwana. Angalieni, kama udongo ulivyo katika mkono wa mfinyanzi, ndivyo mlivyo ninyi katika mkono wangu, Ee nyumba ya Israeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Enyi Waisraeli! Je, mimi Mwenyezi-Mungu siwezi kuwafanya nyinyi kama alivyofanya mfinyanzi huyu? Jueni kuwa kama ulivyo udongo mikononi mwa mfinyanzi, ndivyo nyinyi mlivyo mikononi mwangu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Ee nyumba ya Israeli, je, siwezi kuwafanyia kama huyu mfinyanzi afanyavyo?” Asema BWANA. “Kama vile udongo ulivyo katika mikono ya mfinyanzi, ndivyo mlivyo katika mkono wangu, Ee nyumba ya Israeli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Ee nyumba ya Israeli, je, siwezi kuwafanyia kama huyu mfinyanzi afanyavyo?” asema bwana. “Kama vile udongo ulivyo katika mikono ya mfinyanzi, ndivyo mlivyo katika mkono wangu, ee nyumba ya Israeli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ee nyumba ya Israeli, je! Siwezi mimi kuwatendea ninyi vile vile kama mfinyanzi huyu alivyotenda? Asema BWANA. Angalieni, kama udongo ulivyo katika mkono wa mfinyanzi, ndivyo mlivyo ninyi katika mkono wangu, Ee nyumba ya Israeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Enyi Waisraeli! Je, mimi Mwenyezi-Mungu siwezi kuwafanya nyinyi kama alivyofanya mfinyanzi huyu? Jueni kuwa kama ulivyo udongo mikononi mwa mfinyanzi, ndivyo nyinyi mlivyo mikononi mwangu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kama huyu mfinyanzi nami siwezi kuwafanyizia ninyi mlio mlango wa Isiraeli? ndivyo, asemavyo Bwana. Tazameni: kama udongo ulivyo mkononi mwa mfinyanzi. ndivyo, ninyi mlio mlango wa Isiraeli mlivyo mkononi mwangu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ee nyumba ya Israeli, je! Siwezi mimi kuwatendea ninyi vile vile kama mfinyanzi huyu alivyotenda? Asema BWANA. Angalieni, kama udongo ulivyo katika mkono wa mfinyanzi, ndivyo mlivyo ninyi katika mkono wangu, Ee nyumba ya Israeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Enyi Waisraeli! Mimi siwezi kuwafanya ninyi kama mufinyanzi huyu anavyofanya? –Ni ujumbe wa Yawe.– Mujue kwamba kama vile udongo unavyokuwa katika mikono ya mufinyanzi, ndivyo ninyi munavyokuwa katika mikono yangu.