Jeremiah 19:11 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
na kuwaambia kuwa mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi, nasema hivi: Ndivyo nitakavyovunjavunja watu hawa na mji huu kama vile mtu avunjavyo chombo cha mfinyanzi, hata kisiweze kamwe kutengenezwa tena. Watu watazikwa Tofethi, kwa sababu hapatakuwa na mahali pengine pa kuzikia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
uwaambie, ‘Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: Nitalivunja taifa hili na mji huu kama gudulia hili la mfinyanzi lilivyovunjwa, nalo haliwezi kutengenezeka tena. Watawazika waliokufa huko Tofethi hata isiwepo nafasi zaidi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na kuwaambia, Bwana wa majeshi asema hivi, Hivyo ndivyo nitakavyowavunja watu hawa, na mji huu, kama mtu avunjavyo chombo cha mfinyanzi, kisichoweza kutengenezwa tena na kuwa kizima; nao watazika watu katika Tofethi hata hapatabaki mahali pa kuzika.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
na kuwaambia kuwa mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi, nasema hivi: Ndivyo nitakavyovunjavunja watu hawa na mji huu kama vile mtu avunjavyo chombo cha mfinyanzi, hata kisiweze kamwe kutengenezwa tena. Watu watazikwa Tofethi, kwa sababu hapatakuwa na mahali pengine pa kuzikia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
uwaambie, ‘Hili ndilo BWANA Mwenye Nguvu Zote asemalo: Nitalivunja taifa hili na mji huu kama gudulia hili la mfinyanzi lilivyovunjwa, nalo haliwezi kutengenezeka tena. Watawazika waliokufa huko Tofethi hata isiwepo nafasi zaidi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
uwaambie, ‘Hili ndilo bwana Mwenye Nguvu Zote asemalo: Nitalivunja taifa hili na mji huu kama gudulia hili la mfinyanzi lilivyovunjwa, nalo haliwezi kutengenezeka tena. Watawazika waliokufa huko Tofethi hata isiwepo nafasi zaidi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na kuwaambia, BWANA wa majeshi asema hivi, Hivyo ndivyo nitakavyowavunja watu hawa, na mji huu, kama mtu avunjavyo chombo cha mfinyanzi, kisichoweza kutengenezwa tena na kuwa kizima; nao watazika watu katika Tofethi hata pasibaki mahali pa kuzikia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
na kuwaambia kuwa mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi, nasema hivi: Ndivyo nitakavyovunjavunja watu hawa na mji huu kama vile mtu avunjavyo chombo cha mfinyanzi, hata kisiweze kamwe kutengenezwa tena. Watu watazikwa Tofethi, kwa sababu hapatakuwa na mahali pengine pa kuzikia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
ukiwaambia: Hivi ndivyo, Bwana Mwenye vikosi anavyosema: Hivi ndivyo, nitakavyowavunja walio wa ukoo huu nao mji huu, kama mtu anavyokivunja chombo cha mfinyanzi kisichowezekana kuwa kizima tena. Nako Tofeti ndiko, watakakozikia, kwa kukosa pengine pa kuzikia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na kuwaambia, BWANA wa majeshi asema hivi, Hivyo ndivyo nitakavyowavunja watu hawa, na mji huu, kama mtu avunjavyo chombo cha mfinyanzi, kisichoweza kutengenezwa tena na kuwa kizima; nao watazika watu katika Tofethi hata hapatabaki mahali pa kuzika.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
na kuwaambia kwamba: Yawe wa majeshi, anasema hivi: Nitavunjavunja watu hawa na muji huu sawa vile mutu anavyovunja chombo cha mufinyanzi, hata kisiweze kutengenezwa tena. Watu watazikwa Tofeti, kwa sababu hapatakuwa pahali pengine pa kuzikia.