Jeremiah 19:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nyumba za Yerusalemu na ikulu za wafalme wa Yuda, naam, nyumba zote ambazo juu ya paa zake watu walifukiza ubani kwa sayari za mbinguni, na kumiminia miungu mingine tambiko za divai, zote zitatiwa unajisi kama Tofethi.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nyumba zilizo Yerusalemu na zile za wafalme wa Yuda zitatiwa unajisi kama mahali hapa, Tofethi: yaani nyumba zote ambazo walifukiza uvumba juu ya mapaa yake kwa jeshi lote la angani, na kumimina dhabihu za vinywaji kwa miungu mingine.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na nyumba za Yerusalemu, na nyumba za wafalme wa Yuda, zilizotiwa unajisi, zitakuwa kama mahali pa Tofethi; naam, nyumba zote ambazo juu ya dari zake wamelifukizia uvumba jeshi lote la mbinguni, na kuwamiminia miungu mingine sadaka za kunywewa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nyumba za Yerusalemu na ikulu za wafalme wa Yuda, naam, nyumba zote ambazo juu ya paa zake watu walifukiza ubani kwa sayari za mbinguni, na kumiminia miungu mingine tambiko za divai, zote zitatiwa unajisi kama Tofethi.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nyumba zilizoko Yerusalemu na zile za wafalme wa Yuda zitatiwa unajisi kama mahali hapa, yaani, Tofethi. Nyumba zote ambazo walifukiza uvumba juu ya mapaa yake kwa jeshi lote la angani na kumimina dhabihu ya kinywaji kwa miungu mingine.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nyumba zilizoko Yerusalemu na zile za wafalme wa Yuda zitatiwa unajisi kama mahali hapa, Tofethi: yaani nyumba zote ambazo walifukiza uvumba juu ya mapaa yake kwa jeshi lote la angani, na kumimina dhabihu za vinywaji kwa miungu mingine.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na nyumba za Yerusalemu, na nyumba za wafalme wa Yuda, zilizotiwa unajisi, zitakuwa kama mahali pa Tofethi; naam, nyumba zote ambazo juu ya madari yake wamelifukizia uvumba jeshi lote la mbinguni, na kuwamiminia miungu mingine sadaka za kunywewa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nyumba za Yerusalemu na ikulu za wafalme wa Yuda, naam, nyumba zote ambazo juu ya paa zake watu walifukiza ubani kwa sayari za mbinguni, na kumiminia miungu mingine tambiko za divai, zote zitatiwa unajisi kama Tofethi.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, nyumba za Yerusalemu na nyumba za wafalme wa Yuda zitakapokuwa zimetiwa uchafu kama mahali pa Tofeti, Zitakazokuwa hivyo ni nyumba zote, walimovukizia vikosi vyote vya mbinguni madarini juu, walimomwagia miungu mingine vinywaji vya tambiko.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na nyumba za Yerusalemu, na nyumba za wafalme wa Yuda, zilizotiwa unajisi, zitakuwa kama mahali pa Tofethi; naam, nyumba zote ambazo juu ya dari zake wamelifukizia uvumba jeshi lote la mbinguni, na kuwamiminia miungu mingine sadaka za kunywewa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nyumba za Yerusalema na nyumba za wafalme wa Yuda, ndizo nyumba zote ambazo juu ya paa zao watu walifukiza ubani kwa kutambikia makundi ya nyota, na kuitolea miungu mingine sadaka za divai, zote zitageuzwa kuwa chafu kama Tofeti.