Jeremiah 19:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Utasema hivi: Sikilizeni neno la Mwenyezi-Mungu enyi wafalme wa Yuda na wakazi wa Yerusalemu. Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi: Kweli ninaleta maafa mabaya mahali hapa, hata kila mmoja atakayesikia habari zake, atapigwa na bumbuazi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
nawe useme, ‘Sikieni neno la Mwenyezi Mungu, enyi wafalme wa Yuda na watu wa Yerusalemu. Hili ndilo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wa Israeli, asemalo: Sikilizeni! Nitaleta maafa mahali hapa, ambayo yatafanya masikio ya kila mmoja atakayesikia habari zake yawashe.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ukisema, Lisikieni neno la Bwana, enyi wafalme wa Yuda, na wenyeji wa Yerusalemu; Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli asema hivi, Angalieni, nitaleta mabaya juu ya mahali hapa, ambayo mtu ye yote akisikia habari yake, masikio yake yatawaka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Utasema hivi: Sikilizeni neno la Mwenyezi-Mungu enyi wafalme wa Yuda na wakazi wa Yerusalemu. Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi: Kweli ninaleta maafa mabaya mahali hapa, hata kila mmoja atakayesikia habari zake, atapigwa na bumbuazi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
nawe useme, ‘Sikieni neno la BWANA, enyi wafalme wa Yuda na watu wa Yerusalemu. Hili ndilo BWANA Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli asemalo: Sikilizeni! Nitaleta maafa mahali hapa ambayo yatafanya masikio ya kila mmoja atakayesikia habari zake yawashe.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
nawe useme, ‘Sikieni neno la bwana, enyi wafalme wa Yuda na watu wa Yerusalemu. Hili ndilo bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: Sikilizeni! Nitaleta maafa mahali hapa, ambayo yatafanya masikio ya kila mmoja atakayesikia habari zake yawashe.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ukisema, Lisikieni neno la BWANA, enyi wafalme wa Yuda, na wenyeji wa Yerusalemu; BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli asema hivi, Angalieni, nitaleta mabaya juu ya mahali hapa, ambayo mtu yeyote akisikia habari yake, masikio yake yatawasha.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Utasema hivi: Sikilizeni neno la Mwenyezi-Mungu enyi wafalme wa Yuda na wakazi wa Yerusalemu. Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi: Kweli ninaleta maafa mabaya mahali hapa, hata kila mmoja atakayesikia habari zake, atapigwa na bumbuazi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Uwaambie: Lisikilizeni neno la Bwana, ninyi wafalme wa Yuda nanyi mkaao Yerusalemu! Hivi ndivyo, Bwana Mwenye vikosi, Mungu wa Isiraeli, anavyosema: Mtaniona, nikipaletea mahali hapa mabaya; kila atakayeyasikia masikio yake yatavuma.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ukisema, Lisikieni neno la BWANA, enyi wafalme wa Yuda, na wenyeji wa Yerusalemu; BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli asema hivi, Angalieni, nitaleta mabaya juu ya mahali hapa, ambayo mtu ye yote akisikia habari yake, masikio yake yatawaka.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Utasema hivi: Musikilize neno la Yawe, enyi wafalme wa Yuda nanyi wakaaji wa Yerusalema. Yawe wa majeshi, Mungu wa Israeli, anasema hivi: Kweli ninaleta hasara kwenye nafasi hii, hata kila mumoja atakayesikia habari ile, atastajabu.