Jeremiah 19:4 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa maana watu wameniacha mimi na kupatia unajisi mahali hapa kwa kufukizia ubani miungu mingine; miungu ambayo wao wenyewe, wazee wao wala wafalme wa Yuda hawajapata kuijua. Pia wamepajaza mahali hapa damu ya watu wasio na hatia,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa kuwa wameniacha na kupafanya mahali hapa kuwa pa miungu ya kigeni. Wamefukizia uvumba miungu ambayo wao, wala baba zao, wala wafalme wa Yuda kamwe hawakuijua, nao wamelijaza eneo hili kwa damu isiyo na hatia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa sababu wameniacha mimi, nao wamepafanya mahali hapa kuwa mahali pageni, nao hapa wamewafukizia uvumba miungu mingine wasiowajua, wala wao, wala baba zao, wala wafalme wa Yuda; nao wamepajaza mahali hapa damu ya wasio na hatia;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa maana watu wameniacha mimi na kupatia unajisi mahali hapa kwa kufukizia ubani miungu mingine; miungu ambayo wao wenyewe, wazee wao wala wafalme wa Yuda hawajapata kuijua. Pia wamepajaza mahali hapa damu ya watu wasio na hatia,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa kuwa wameniacha na kupafanya mahali hapa kuwa pa miungu ya kigeni, wameiteketezea sadaka miungu ambayo wao wala baba zao wala wafalme wa Yuda kamwe hawakuijua, nao wamelijaza eneo hili kwa damu isiyo na hatia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa kuwa wameniacha na kupafanya mahali hapa kuwa pa miungu ya kigeni. Wameiteketezea sadaka miungu ambayo wao wala baba zao wala wafalme wa Yuda kamwe hawakuijua, nao wamelijaza eneo hili kwa damu isiyo na hatia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa sababu wameniacha mimi, nao wamepafanya mahali hapa kuwa mahali pageni, nao hapa wamewafukizia uvumba miungu mingine wasiowajua, wala wao, wala baba zao, wala wafalme wa Yuda; nao wamepajaza mahali hapa damu ya wasio na hatia;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa maana watu wameniacha mimi na kupatia unajisi mahali hapa kwa kufukizia ubani miungu mingine; miungu ambayo wao wenyewe, wazee wao wala wafalme wa Yuda hawajapata kuijua. Pia wamepajaza mahali hapa damu ya watu wasio na hatia,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ni kwa sababu wameniacha, mahali hapa wakampa mgeni, wakavukizia hapa miungu mingine, wasiyoijua wenyewe, wala baba zao, wala wafalme wa Yuda, wakapajaza mahali hapa damu zao wasiokosa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa sababu wameniacha mimi, nao wamepafanya mahali hapa kuwa mahali pageni, nao hapa wamewafukizia uvumba miungu mingine wasiowajua, wala wao, wala baba zao, wala wafalme wa Yuda; nao wamepajaza mahali hapa damu ya wasio na hatia;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana watu wameniacha mimi na kuchafua nafasi hii kwa kufukizia miungu mingine ubani; miungu ambayo wao wenyewe, babu zao wala wafalme wa Yuda hawaijui. Zaidi ya ile wamejaza pahali hapa damu ya watu wasiokuwa na kosa,