Jeremiah 19:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maadui watauzingira na kujaribu kuwaua watu wake. Watasababisha hali mbaya sana mjini humo hata watu watawala watoto wao wa kike na wa kiume, na kila mtu atamla mwenzake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nitawafanya wao kula nyama ya wana wao wa kiume na wa kike; kila mmoja atakula nyama ya mwenzake wakati wa dhiki ya kuzingirwa na jeshi la adui wanaotafuta uhai wao.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nami nitawalazimisha kula nyama ya wana wao, na nyama ya binti zao, nao watakula kila mmoja nyama ya rafiki yake, wakati wa mazingira na dhiki, ambayo adui zao, na watu wale watafutao roho zao, watawadhiikisha.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maadui watauzingira na kujaribu kuwaua watu wake. Watasababisha hali mbaya sana mjini humo hata watu watawala watoto wao wa kike na wa kiume, na kila mtu atamla mwenzake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nitawafanya wao kula nyama ya wana wao na binti zao, kila mmoja atakula nyama ya mwenzake wakati wa dhiki ya kuzungukwa na jeshi lililowekwa juu yao na adui wanaotafuta uhai wao.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nitawafanya wao kula nyama ya wana wao na binti zao; kila mmoja atakula nyama ya mwenzake wakati wa dhiki ya kuzungukwa na jeshi lililowekwa juu yao na adui wanaotafuta uhai wao.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nami nitawalazimisha kula nyama ya wana wao, na nyama ya binti zao, nao watakula kila mmoja nyama ya rafiki yake, wakati wa mazingira na dhiki, ambayo adui zao, na watu wale watafutao roho zao, watawatesa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maadui watauzingira na kujaribu kuwaua watu wake. Watasababisha hali mbaya sana mjini humo hata watu watawala watoto wao wa kike na wa kiume, na kila mtu atamla mwenzake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nitawalisha nyama za wana wao wa kiume na nyama za wana wao wa kike, watazila kila mtu nyama za mwenziwe kwa kusongeka na kwa kuhangaika, adui zao wanaozitaka roho zao wakiwahangaisha.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nami nitawalazimisha kula nyama ya wana wao, na nyama ya binti zao, nao watakula kila mmoja nyama ya rafiki yake, wakati wa mazingira na dhiki, ambayo adui zao, na watu wale watafutao roho zao, watawadhiikisha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Waadui wao wanavizia maisha yao watauzunguka muji ule kwa vita. Wataleta taabu na masumbuko hata watu watakula wenzao. Nitawafanya wakule miili ya wana na wabinti zao.