Jeremiah 2:11 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwamba kuna taifa lililowahi kubadilisha miungu yake ingawa miungu hiyo si miungu! Lakini watu wangu wameniacha mimi, utukufu wao, wakafuata miungu isiyofaa kitu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Je, taifa limebadili miungu yake wakati wowote? (Hata ingawa hao si miungu kamwe.) Lakini watu wangu wamebadili Utukufu wao kwa sanamu batili.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Je! Taifa wamebadili miungu yao, ingawa siyo miungu? Lakini watu wangu wameubadili utukufu wao kwa ajili ya kitu kisichofaidia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
kwamba kuna taifa lililowahi kubadilisha miungu yake ingawa miungu hiyo si miungu! Lakini watu wangu wameniacha mimi, utukufu wao, wakafuata miungu isiyofaa kitu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Je, taifa limebadili miungu yake wakati wo wote? (Hata ingawa hao si miungu kamwe.) Lakini watu wangu wamebadili Utukufu wao kwa sanamu zisizofaa kitu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Je, taifa limebadili miungu yake wakati wowote? (Hata ingawa hao si miungu kamwe.) Lakini watu wangu wamebadili Utukufu wao kwa sanamu zisizofaa kitu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Je! Taifa wamebadili miungu yao, ingawa siyo miungu? Lakini watu wangu wameubadili utukufu wao kwa ajili ya kitu kisichofaidia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwamba kuna taifa lililowahi kubadilisha miungu yake ingawa miungu hiyo si miungu! Lakini watu wangu wameniacha mimi, utukufu wao, wakafuata miungu isiyofaa kitu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mwone, kama liko taifa lililoiacha miungu ya kwao na kufuata mingine, nayo siyo miungu! Nao walio ukoo wangu wameuacha utukufu wao wakifuata yasiyofaa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Je! Taifa wamebadili miungu yao, ingawa siyo miungu? Lakini watu wangu wameubadili utukufu wao kwa ajili ya kitu kisichofaidia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kuna taifa ambalo limekwisha kubadilisha miungu yao ingawa miungu hiyo si miungu? Lakini watu wangu wameniacha mimi, utukufu wao, wakafuata miungu isiyokuwa na faida yoyote.