Jeremiah 2:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana, watu wangu wametenda maovu mawili; wameniacha mimi niliye chemchemi ya maji ya uhai, wakajichimbia visima vyao wenyewe, visima vyenye nyufa, visivyoweza kuhifadhi maji.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Watu wangu wametenda dhambi mbili: Wameniacha mimi, niliye chemchemi ya maji yaliyo hai, nao wamejichimbia visima vyao wenyewe, visima vilivyobomoka, visivyoweza kuhifadhi maji.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana watu wangu hawa wametenda maovu mawili; wameniacha mimi, niliye chemchemi ya maji ya uzima, wamejichimbia mabirika, mabirika yavujayo, yasiyoweza kuweka maji.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana, watu wangu wametenda maovu mawili; wameniacha mimi niliye chemchemi ya maji ya uhai, wakajichimbia visima vyao wenyewe, visima vyenye nyufa, visivyoweza kuhifadhi maji.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Watu wangu wametenda dhambi mbili: Wameniacha mimi, niliye chemchemi ya maji yaliyo hai, nao wamejichimbia visima vyao wenyewe, visima vilivyobomoka visivyoweza kuhifadhi maji.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Watu wangu wametenda dhambi mbili: Wameniacha mimi, niliye chemchemi ya maji yaliyo hai, nao wamejichimbia visima vyao wenyewe, visima vilivyobomoka, visivyoweza kuhifadhi maji.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana watu wangu hawa wametenda maovu mawili; wameniacha mimi, niliye chemchemi ya maji ya uzima, wamejichimbia visima, visima vyenye nyufa visivyoweza kuweka maji.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana, watu wangu wametenda maovu mawili; wameniacha mimi niliye chemchemi ya maji ya uhai, wakajichimbia visima vyao wenyewe, visima vyenye nyufa, visivyoweza kuhifadhi maji.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani walio ukoo wangu wamefanya mabaya mawili: wameniacha mimi niliye kisima chenye maji ya uzima, kisha wakajichimbia visima vingine, navyo ni visima vyenye nyufa visivyoweza kushika maji.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana watu wangu hawa wametenda maovu mawili; wameniacha mimi, niliye chemchemi ya maji ya uzima, wamejichimbia mabirika, mabirika yavujayo, yasiyoweza kuweka maji.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wangu wametenda maovu mawili; wameniacha mimi ninayekuwa chemichemi ya maji ya uzima, wakajichimbia visima vyao wenyewe, visima vyenye nyufa, visivyoweza kuchunga maji.