Jeremiah 2:19 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Uovu wako utakuadhibu; na uasi wako utakuhukumu. Ujue na kutambua kuwa ni vibaya mno kuniacha mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, na kuondoa uchaji wangu ndani yako. Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nimesema.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Uovu wako utakuadhibu; kurudi nyuma kwako kutakukemea. Basi kumbuka, utambue jinsi lilivyo jambo ovu na chungu kwako unapomwacha Mwenyezi Mungu, Mungu wako, na kutokuwa na hofu yangu,” asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Uovu wako mwenyewe utakurudi, maasi yako yatakukaripia; ujue, basi, ukaone, ya kuwa ni jambo baya sana na uchungu, kuwa umemwacha Bwana, Mungu wako, na ya kuwa moyoni mwako hamna kunihofu, asema Bwana, Bwana wa majeshi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Uovu wako utakuadhibu; na uasi wako utakuhukumu. Ujue na kutambua kuwa ni vibaya mno kuniacha mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, na kuondoa uchaji wangu ndani yako. Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nimesema.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Uovu wako utakuadhibu; kurudi nyuma kwako kutakukemea. Basi kumbuka, utambue jinsi lilivyo ovu na chungu kwako unapomwacha BWANA Mungu wako na kutokuwa na hofu yangu,” asema Bwana, BWANA Mwenye Nguvu Zote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Uovu wako utakuadhibu; kurudi nyuma kwako kutakukemea. Basi kumbuka, utambue jinsi lilivyo ovu na chungu kwako unapomwacha bwana Mwenyezi Mungu wako na kutokuwa na hofu yangu,” asema Bwana, bwana Mwenye Nguvu Zote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Uovu wako mwenyewe utakurudi, maasi yako yatakukaripia; ujue, basi, ukaone, ya kuwa ni jambo baya sana na uchungu, kuwa umemwacha BWANA, Mungu wako, na ya kuwa moyoni mwako hamna kunihofu, asema Bwana, BWANA wa majeshi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Uovu wako utakuadhibu; na uasi wako utakuhukumu. Ujue na kutambua kuwa ni vibaya mno kuniacha mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, na kuondoa uchaji wangu ndani yako. Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nimesema.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ubaya wako ndio unaokupiga, ubishi wako ndio unaokupatiliza. Yajue, yatazame, ya kuwa kumwacha Bwana Mungu wako ndiko kubaya kwenye uchungu! Nawe hukumwogopa kamwe. Ndivyo, asemavyo Bwana Mungu wako Mwenye vikosi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Uovu wako mwenyewe utakurudi, maasi yako yatakukaripia; ujue, basi, ukaone, ya kuwa ni jambo baya sana na uchungu, kuwa umemwacha BWANA, Mungu wako, na ya kuwa moyoni mwako hamna kunihofu, asema Bwana, BWANA wa majeshi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Uovu wako utakuazibu; na uasi wako utakuhukumu. Ujue na kutambua kwamba ni vibaya sana kuacha Bwana wako Yawe, Mungu wako, na kutokuwa na woga wangu ndani yako. –Ni ujumbe wa Bwana wetu Yawe wa majeshi.–