Jeremiah 2:24 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
kama pundamwitu aliyezoea jangwani. Katika tamaa yake hunusanusa upepo; nani awezaye kuizuia hamu yake? Amtakaye hana haja ya kujisumbua; wakati wake ufikapo watampata tu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
punda-mwitu aliyezoea jangwa, anayenusa upepo katika tamaa yake kubwa: wakati wake wa kuhitaji mbegu ni nani awezaye kumzuia? Madume yoyote yanayomfuatilia hayana haja ya kujichosha; wakati wa kupandwa kwake yatampata tu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
punda wa mwitu aliyeizoelea nyika, avutaye pumzi za upepo katika tamaa yake; katika wakati wake ni nani awezaye kumgeuza? Wote wamtafutao hawatajichokesha nafsi zao; katika mwezi wake watamwona.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
kama pundamwitu aliyezoea jangwani. Katika tamaa yake hunusanusa upepo; nani awezaye kuizuia hamu yake? Amtakaye hana haja ya kujisumbua; wakati wake ufikapo watampata tu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
punda-mwitu aliyezoea jangwa, anayenusa upepo, katika tamaa yake kubwa: akiwa katika wakati wake wa kuhitaji mbegu ni nani awezae kumzuia? Madume yo yote yanayomfuatilia hayana haja ya kujichosha; wakati wa kupandwa kwake watampata tu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
punda-mwitu aliyezoea jangwa, anayenusa upepo katika tamaa yake kubwa: katika wakati wake wa kuhitaji mbegu ni nani awezaye kumzuia? Madume yoyote yanayomfuatilia hayana haja ya kujichosha; wakati wa kupandwa kwake watampata tu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
punda wa mwitu aliyeizoelea nyika, avutaye pumzi za upepo katika tamaa yake; katika wakati wake ni nani awezaye kumgeuza? Wote wamtafutao hawatajichosha nafsi zao; katika mwezi wake watamwona.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
kama pundamwitu aliyezoea jangwani. Katika tamaa yake hunusanusa upepo; nani awezaye kuizuia hamu yake? Amtakaye hana haja ya kujisumbua; wakati wake ufikapo watampata tu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ukawa kama kihongwe cha kike azoeaye nyika, naye hutwetea upepo kwa kukimbizwa na tamaa ya roho yake; tena yuko nani awezaye kuzituliza nyege zake? Lakini amtafutaye hajichokeshi: mwezi wake unapotimia, humwona upesi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
punda wa mwitu aliyeizoelea nyika, avutaye pumzi za upepo katika tamaa yake; katika wakati wake ni nani awezaye kumgeuza? Wote wamtafutao hawatajichokesha nafsi zao; katika mwezi wake watamwona.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
kama punda dike wa pori aliyezoea jangwa. Katika tamaa yake ananusanusa upepo; nani anayeweza kumuzuiza katika hamu yake? Dume anayemutamani hahitaji kujisumbua; wakati wake unapofika watamupata tu.