Jeremiah 2:28 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Lakini iko wapi miungu yako uliyojifanyia? Iinuke basi, kama inaweza kukusaidia, wakati unapokuwa katika shida. Ee Yuda, idadi ya miungu yako ni sawa na idadi ya miji yako!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Iko wapi basi ile miungu mliyojitengenezea? Yenyewe na ije kama inaweza kuwaokoa wakati mko katika taabu! Kwa maana mna miungu mingi kama mlivyo na miji, ee Yuda.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini wako wapi miungu yako ulioifanya? Na wasimame hao, kama wakiweza kukuokoa wakati wa taabu yako; kwa maana hesabu ya miungu yako ni sawasawa na hesabu ya miji yako, Ee Yuda.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Lakini iko wapi miungu yako uliyojifanyia? Iinuke basi, kama inaweza kukusaidia, wakati unapokuwa katika shida. Ee Yuda, idadi ya miungu yako ni sawa na idadi ya miji yako!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Iko wapi basi ile miungu mliyojitengenezea? Yenyewe na ije kama inaweza kuwaokoa wakati mnapokuwa katika taabu! Kwa maana mna miungu mingi kama mlivyo na miji, Ee Yuda.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Iko wapi basi ile miungu mliyojitengenezea? Yenyewe na ije kama inaweza kuwaokoa wakati mko katika taabu! Kwa maana mna miungu mingi kama mlivyo na miji, ee Yuda.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini wako wapi miungu yako ulioifanya? Na wasimame hao, kama wakiweza kukuokoa wakati wa taabu yako; kwa maana hesabu ya miungu yako ni sawa na hesabu ya miji yako, Ee Yuda.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Lakini iko wapi miungu yako uliyojifanyia? Iinuke basi, kama inaweza kukusaidia, wakati unapokuwa katika shida. Ee Yuda, idadi ya miungu yako ni sawa na idadi ya miji yako!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Basi, miungu yako, uliyojifanyizia, iko wapi? Na iinuke, kama inaweza kukuokoa, unapopatwa na mabaya! Kama miji yako ilivyo mingi, ndivyo, nayo miungu yako, wewe Yuda, ilivyo mingi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini wako wapi miungu yako ulioifanya? Na wasimame hao, kama wakiweza kukuokoa wakati wa taabu yako; kwa maana hesabu ya miungu yako ni sawasawa na hesabu ya miji yako, Ee Yuda.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini iko wapi ile miungu yenu muliyojifanyia? Basi kama inaweza, isimame iwasaidie, wakati munapokuwa katika shida. Ee ninyi watu wa Yuda, hesabu ya miungu yenu ni sawa na hesabu ya miji yenu!