Jeremiah 2:31 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Enyi watu! Sikilizeni ninachosema mimi Mwenyezi-Mungu: Je, nimekuwa jangwa kwa Israeli au nchi yenye giza nene? Kwa nini basi watu wangu waseme: ‘Sisi tu watu huru; hatutakuja kwako tena!’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Enyi wa kizazi hiki, tafakarini neno la Mwenyezi Mungu: “Je, nimekuwa jangwa kwa Israeli au nchi ya giza nene? Kwa nini watu wangu wanasema, ‘Sisi tuko huru kuzurura, hatutarudi kwako tena’?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ee kizazi litazameni neno la Bwana. Je! Nimekuwa jangwa kwa Israeli? Au nchi yenye giza kuu? Mbona watu wangu wanasema, Sisi tumetoroka, hatutaki kuja kwako tena?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Enyi watu! Sikilizeni ninachosema mimi Mwenyezi-Mungu: Je, nimekuwa jangwa kwa Israeli au nchi yenye giza nene? Kwa nini basi watu wangu waseme: ‘Sisi tu watu huru; hatutakuja kwako tena!’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Enyi wa kizazi hiki, kumbukeni neno la BWANA: “Je, nimekuwa jangwa kwa Israeli au nchi ya giza kuu? Kwa nini watu wangu wanasema, ‘Sisi tuko huru kuzurura, hatutarudi kwako tena’?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Enyi wa kizazi hiki, tafakarini neno la bwana: “Je, nimekuwa jangwa kwa Israeli au nchi ya giza kuu? Kwa nini watu wangu wanasema, ‘Sisi tuko huru kuzurura, hatutarudi kwako tena’?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ee kizazi, litazameni neno la BWANA. Je! Nimekuwa jangwa kwa Israeli? Au nchi yenye giza kuu? Mbona watu wangu wanasema, Sisi tumetoroka, hatutaki kuja kwako tena?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Enyi watu! Sikilizeni ninachosema mimi Mwenyezi-Mungu: Je, nimekuwa jangwa kwa Israeli au nchi yenye giza nene? Kwa nini basi watu wangu waseme: ‘Sisi tu watu huru; hatutakuja kwako tena!’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ninyi mlio uzao mbaya, liangalieni Neno la Bwana! Je? Nimegeuka kuwawia Waisiraeli kama nyika au kama nchi yenye giza? Kwa sababu gani walio ukoo wangu husema: Tumekwisha kujiendea, haturudi kwako tena.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ee kizazi litazameni neno la BWANA. Je! Nimekuwa jangwa kwa Israeli? Au nchi yenye giza kuu? Mbona watu wangu wanasema, Sisi tumetoroka, hatutaki kuja kwako tena?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Enyi watu! Musikilize vile mimi Yawe ninavyosema: Nimekuwa kama vile jangwa au inchi yenye giza kubwa? Kwa nini basi watu wangu wanasema: Sisi tuko watu huru; hatutakurudilia!