Jeremiah 2:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hawakujiuliza: ‘Yuko wapi Mwenyezi-Mungu aliyetutoa nchini Misri, aliyetuongoza nyikani katika nchi ya jangwa na makorongo, nchi kame na yenye giza nene, nchi isiyopitiwa na mtu yeyote, wala kukaliwa na binadamu?’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hawakuuliza, ‘Yuko wapi Mwenyezi Mungu, aliyetupandisha kutoka Misri na kutuongoza kupitia nyika kame, kupitia nchi ya majangwa na mabonde, nchi ya ukame na giza, nchi ambayo hakuna mtu asafiriye ndani yake wala hakuna mtu aishiye humo?’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wala hawakusema, Yuko wapi Bwana, aliyetutoa katika nchi ya Misri; akatuongoza jangwani, katika nchi ya ukame na mashimo, katika nchi ya kiu na ya kivuli cha mauti, katika nchi ambayo ndani yake hapiti mtu, wala haikukaliwa na watu?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hawakujiuliza: ‘Yuko wapi Mwenyezi-Mungu aliyetutoa nchini Misri, aliyetuongoza nyikani katika nchi ya jangwa na makorongo, nchi kame na yenye giza nene, nchi isiyopitiwa na mtu yeyote, wala kukaliwa na binadamu?’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hawakuuliza, ‘Yuko wapi BWANA, aliyetupandisha kutoka Misri na kutuongoza kupitia katika nyika kame, kupitia katika nchi ya majangwa na mabonde, nchi ya ukame na giza, nchi ambayo hakuna mtu asafiriye ndani yake wala hakuna mtu aishiye humo?’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hawakuuliza, ‘Yuko wapi bwana, aliyetupandisha kutoka Misri na kutuongoza kupitia nyika kame, kupitia nchi ya majangwa na mabonde, nchi ya ukame na giza, nchi ambayo hakuna mtu asafiriye ndani yake wala hakuna mtu aishiye humo?’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wala hawakusema, Yuko wapi BWANA, aliyetutoa katika nchi ya Misri; akatuongoza jangwani, katika nchi ya ukame na mashimo, katika nchi ya kiu na ya kivuli cha mauti, katika nchi ambayo ndani yake hapiti mtu, wala haikukaliwa na watu?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hawakujiuliza: ‘Yuko wapi Mwenyezi-Mungu aliyetutoa nchini Misri, aliyetuongoza nyikani katika nchi ya jangwa na makorongo, nchi kame na yenye giza nene, nchi isiyopitiwa na mtu yeyote, wala kukaliwa na binadamu?’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hawakuuliza: Bwana yuko wapi aliyetutoa katika nchi ya Misri, aliyetuongoza nyikani katika nchi zenye jangwa na makorongo, katika nchi kavu ziuazo, katika nchi zisizopitwa na mtu, zisizokaa mtu?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wala hawakusema, Yuko wapi BWANA, aliyetutoa katika nchi ya Misri; akatuongoza jangwani, katika nchi ya ukame na mashimo, katika nchi ya kiu na ya kivuli cha mauti, katika nchi ambayo ndani yake hapiti mtu, wala haikukaliwa na watu?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hawakujiuliza hivi: Yuko wapi Yawe aliyetuondoa katika inchi ya Misri, aliyetuongoza katika mbuga, katika inchi ya jangwa na mashimo, inchi inayokauka na yenye giza kubwa, inchi isiyopitiwa na mutu yeyote, wala kukaliwa na mwanadamu?