Jeremiah 2:8 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nao makuhani hawakujiuliza: ‘Yuko wapi Mwenyezi-Mungu?’ Wataalamu wa sheria hawakunijua, viongozi wa watu waliniasi; manabii nao walitabiri kwa jina la Baali na kuabudu sanamu zisizo na faida yoyote.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Makuhani hawakuuliza, ‘Yuko wapi Mwenyezi Mungu?’ Wale wanaoshughulikia sheria hawakunijua mimi; viongozi waliasi dhidi yangu. Manabii walitabiri kwa jina la Baali, wakifuata sanamu batili.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Makuhani hawakusema, Yuko wapi Bwana? Wala wana-sheria hawakunijua; wachungaji nao waliniasi, nao manabii walitoa unabii kwa Baali, wakafuata mambo yasiyofaidia kitu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nao makuhani hawakujiuliza: ‘Yuko wapi Mwenyezi-Mungu?’ Wataalamu wa sheria hawakunijua, viongozi wa watu waliniasi; manabii nao walitabiri kwa jina la Baali na kuabudu sanamu zisizo na faida yoyote.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Makuhani hawakuuliza, ‘Yuko wapi BWANA?’ Wale wanaoshughulikia sheria hawakunijua mimi; viongozi waliasi dhidi yangu. Manabii walitabiri kwa jina la Baali, wakifuata sanamu zisizofaa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Makuhani hawakuuliza, ‘Yuko wapi bwana?’ Wale wanaoshughulikia sheria hawakunijua mimi; viongozi waliasi dhidi yangu. Manabii walitabiri kwa jina la Baali, wakifuata sanamu zisizofaa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Makuhani hawakusema, Yuko wapi BWANA? Wala wanasheria hawakunijua; wachungaji nao waliniasi, nao manabii walitoa unabii kwa Baali, wakafuata mambo yasiyofaidia kitu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nao makuhani hawakujiuliza: ‘Yuko wapi Mwenyezi-Mungu?’ Wataalamu wa sheria hawakunijua, viongozi wa watu waliniasi; manabii nao walitabiri kwa jina la Baali na kuabudu sanamu zisizo na faida yoyote.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Watambikaji hawakuuliza: Bwana yuko wapi? Wala wenye kazi za Maonyo hawakunijua, wabaya wakanikosea, wafumbuaji wakafumbua mambo ya Baali, wakayafuata yasiyofaa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Makuhani hawakusema, Yuko wapi BWANA? Wala wana-sheria hawakunijua; wachungaji nao waliniasi, nao manabii walitoa unabii kwa Baali, wakafuata mambo yasiyofaidia kitu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nao makuhani hawakujiuliza hivi: Yuko wapi Yawe? Wafundi wa sheria hawakunijua, viongozi wa watu waliniasi; manabii nao walitabiri kwa jina la Bali na kuabudu sanamu zisizokuwa na faida yoyote.