Jeremiah 20:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nasikia wengi wakinongona juu yangu. Wananipanga jina: “Kitisho kila upande!” Wengine wanasema: “Nendeni mkamshtaki! Na tumshtaki!” Hata rafiki zangu wote wapenzi wanangojea tu nianguke! Wanasema “Labda atadanganyika, nasi tutalipiza kisasi.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ninasikia minong’ono mingi, “Hofu iko pande zote! Mshtakini! Twendeni tumshtaki!” Rafiki zangu wote wananisubiri niteleze, wakisema, “Labda atadanganyika; kisha tutamshinda na kulipiza kisasi juu yake.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana nimesikia mashutumu ya watu wengi; hofu ziko pande zote. Rafiki zangu wote, wanaonivizia nisite, husema, Mshitaki, nasi tutamshitaki, huenda akahadaika, nasi tutamshinda, tutajilipiza kisasi kwake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nasikia wengi wakinong'ona juu yangu. Wananipanga jina: “Kitisho kila upande!” Wengine wanasema: “Nendeni mkamshtaki! Na tumshtaki!” Hata rafiki zangu wote wapenzi wanangojea tu nianguke! Wanasema “Labda atadanganyika, nasi tutalipiza kisasi.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ninasikia minong'ono mingi, “Hofu iko pande zote! Mshitakini! Twendeni tumshitaki!” Rafiki zangu wote wananisubiri niteleze, wakisema, “Labda atadanganyika; kisha tutamshinda na kulipiza kisasi juu yake.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ninasikia minong’ono mingi, “Hofu iko pande zote! Mshtakini! Twendeni tumshtaki!” Rafiki zangu wote wananisubiri niteleze, wakisema, “Labda atadanganyika; kisha tutamshinda na kulipiza kisasi juu yake.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana nimesikia shutuma za watu wengi; hofu ziko pande zote. Rafiki zangu wote, wanaonivizia nisite, husema, Mshitaki, nasi tutamshitaki, huenda akahadaika, nasi tutamshinda, tutajilipiza kisasi kwake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nasikia wengi wakinongona juu yangu. Wananipanga jina: “Kitisho kila upande!” Wengine wanasema: “Nendeni mkamshtaki! Na tumshtaki!” Hata rafiki zangu wote wapenzi wanangojea tu nianguke! Wanasema “Labda atadanganyika, nasi tutalipiza kisasi.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani nimesikia wengi, wakinong'onezana kwamba: Anatishwa po pote, mchongeeni! Nasi na tumchongee! Hiyo ni njama yao wote walio rafiki zangu, hunivizia, nianguke, kwamba: Labda atashindwa, tumweze nasi, tupate kujilipiza kwake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana nimesikia mashutumu ya watu wengi; hofu ziko pande zote. Rafiki zangu wote, wanaonivizia nisite, husema, Mshitaki, nasi tutamshitaki, huenda akahadaika, nasi tutamshinda, tutajilipiza kisasi kwake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ninasikia watu wengi wakinisingizia uongo, nao wananipanga jina la Kitisho Kila Pahali! Wengine wanasema: Tumushitaki, Tumushitaki! Rafiki zangu wapenzi wote wanangojea kwa hamu nianguke! Wanasema: Labda atadanganyika, tupate kumunasa na kumulipiza kisasi.