Jeremiah 20:11 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini wewe Mwenyezi-Mungu u pamoja nami kwangu wewe ni kama shujaa wa kutisha; kwa hiyo watesi wangu watajikwaa, na hawataweza kunishinda. Wataaibika kupindukia, maana hawatafaulu. Fedheha yao itakuwa ya daima; kamwe haitasahaulika.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini Mwenyezi Mungu yu pamoja nami kama mpiganaji mwenye nguvu; kwa hiyo watesi wangu watajikwaa, Hawatashinda, nao wataaibika sana; aibu yao haitasahaulika milele.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini Bwana yu pamoja nami, mfano wa shujaa mwenye kutisha; kwa hiyo hao wanaonionea watajikwaa, wala hawatashinda; watatahayarika sana. Kwa sababu hawakutenda kwa akili, wataona aibu ya milele, ambayo haitasahauliwa kamwe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini wewe Mwenyezi-Mungu u pamoja nami kwangu wewe ni kama shujaa wa kutisha; kwa hiyo watesi wangu watajikwaa, na hawataweza kunishinda. Wataaibika kupindukia, maana hawatafaulu. Fedheha yao itakuwa ya daima; kamwe haitasahaulika.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini BWANA yu pamoja nami kama shujaa mwenye nguvu; hivyo washitaki wangu watajikwaa na kamwe hawatashinda. Watashindwa, nao wataaibika kabisa; kukosa adabu kwao hakutasahauliwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini bwana yu pamoja nami kama shujaa mwenye nguvu; hivyo washtaki wangu watajikwaa na kamwe hawatashinda. Watashindwa, nao wataaibika kabisa; kukosa adabu kwao hakutasahauliwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini BWANA yuko pamoja nami, mfano wa shujaa mwenye kutisha; kwa hiyo hao wanaonionea watajikwaa, wala hawatashinda; watatahayarika sana. Kwa sababu hawatafaulu wataona aibu ya milele, ambayo haitasahauliwa kamwe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini wewe Mwenyezi-Mungu u pamoja nami kwangu wewe ni kama shujaa wa kutisha; kwa hiyo watesi wangu watajikwaa, na hawataweza kunishinda. Wataaibika kupindukia, maana hawatafaulu. Fedheha yao itakuwa ya daima; kamwe haitasahaulika.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Bwana yuko pamoja nami kama mpiga vita mwenye nguvu; kwa hiyo wanikimbizao watajikwaa, wasiniweze, watapatwa na soni kabisa, kwani hawaerevuki, soni zao zitakuwa za kale na kale, hazitasahauliwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini BWANA yu pamoja nami, mfano wa shujaa mwenye kutisha; kwa hiyo hao wanaonionea watajikwaa, wala hawatashinda; watatahayarika sana. Kwa sababu hawakutenda kwa akili, wataona aibu ya milele, ambayo haitasahauliwa kamwe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini wewe Yawe uko pamoja nami. Kwangu wewe ni kama shujaa wa kutisha. Kwa hiyo watesaji wangu watajikwaa, nao hawataweza kunishinda. Watafezeheka kabisa, kwa sababu hawatashinda. Haya yao itadumu hata milele, nayo haitasahauliwa.