Jeremiah 20:12 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ee Mwenyezi-Mungu wa majeshi, wewe humthibiti mtu mwadilifu, huona yaliyo moyoni na akilini mwa watu, unijalie kuona ukiwalipiza kisasi, maana kwako nimekiweka kisa changu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, wewe umjaribuye mwenye haki na kupima moyo na nia, hebu nione ukilipiza kisasi juu yao, kwa maana kwako nimeliweka shauri langu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini, Ee Bwana wa majeshi, wewe wawajaribu wenye haki, waona viuno na mioyo, nijalie kuona kisasi chako juu yao; kwa maana nimekufunulia wewe neno langu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ee Mwenyezi-Mungu wa majeshi, wewe humthibiti mtu mwadilifu, huona yaliyo moyoni na akilini mwa watu, unijalie kuona ukiwalipiza kisasi, maana kwako nimekiweka kisa changu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ee BWANA Mwenye Nguvu Zote, wewe umjaribuye mwenye haki na kupima moyo na nia, na nione ukilipiza kisasi juu yao, kwa maana kwako nimeliweka shauri langu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ee bwana Mwenye Nguvu Zote, wewe umjaribuye mwenye haki na kupima moyo na nia, hebu nione ukilipiza kisasi juu yao, kwa maana kwako nimeliweka shauri langu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini, Ee BWANA wa majeshi, wewe wawajaribu wenye haki, waona fikira na mioyo, nijalie kuona kisasi chako juu yao; kwa maana nimekufunulia wewe neno langu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ee Mwenyezi-Mungu wa majeshi, wewe humthibiti mtu mwadilifu, huona yaliyo moyoni na akilini mwa watu, unijalie kuona ukiwalipiza kisasi, maana kwako nimekiweka kisa changu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wewe Bwana unajaribu mwongofu, unayaona mafigo na moyo; na nione, jinsi unavyowalipiza kisasi, kwani nimekusukumia wewe shauri langu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini, Ee BWANA wa majeshi, wewe wawajaribu wenye haki, waona viuno na mioyo, nijalie kuona kisasi chako juu yao; kwa maana nimekufunulia wewe neno langu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ee Yawe wa majeshi, wewe unayemupima mutu wa haki, unayechunguza mioyo na akili ya watu, nione kisasi chako juu yao maana ninakutegemea kwa kunitetea.