Jeremiah 20:4 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana, Mwenyezi-Mungu asema hivi: ‘Tazama, nitakufanya uwe kitisho kwako wewe mwenyewe na kwa rafiki zako wote. Wao watauawa vitani kwa upanga wa maadui zao huku ukiangalia. Nitawatia watu wote wa Yuda mikononi mwa mfalme wa Babuloni, naye atawachukua mateka hadi Babuloni na kuwaua kwa upanga.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa kuwa hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: ‘Nitakufanya uwe tisho kwako na rafiki wako wote; na macho yako mwenyewe yataona wakianguka kwa upanga wa adui zao. Nitawatia Yuda wote mikononi mwa mfalme wa Babeli, ambaye atawachukua mateka na kuwapeleka Babeli, ama awaue kwa upanga.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana Bwana asema hivi, Tazama, nitakufanya kuwa hofu kuu kwa nafsi yako, na kwa rafiki zako wote; nao wataanguka kwa upanga wa adui zao, na macho yako yataona hayo; nami nitatia Yuda yote katika mikono ya mfalme wa Babeli, naye atawachukua mateka mpaka Babeli, na kuwaua kwa upanga.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana, Mwenyezi-Mungu asema hivi: ‘Tazama, nitakufanya uwe kitisho kwako wewe mwenyewe na kwa rafiki zako wote. Wao watauawa vitani kwa upanga wa maadui zao huku ukiangalia. Nitawatia watu wote wa Yuda mikononi mwa mfalme wa Babuloni, naye atawachukua mateka hadi Babuloni na kuwaua kwa upanga.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa kuwa hili ndilo asemalo BWANA: ‘Nitakufanya kuwa hofu kuu kwako wewe mwenyewe na rafiki zako wote, kwa macho yako mwenyewe utawaona wakianguka kwa upanga wa adui zao. Nitawatia Wayahudi wote mikononi mwa mfalme wa Babeli, ambaye atawachukua na kuwapeleka Babeli ama awaue kwa upanga.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa kuwa hili ndilo asemalo bwana: ‘Nitakufanya kuwa hofu kuu kwako wewe mwenyewe na rafiki zako wote, na kwa macho yako mwenyewe utawaona wakianguka kwa upanga wa adui zao. Nitawatia Yuda wote mikononi mwa mfalme wa Babeli, ambaye atawachukua na kuwapeleka Babeli, ama awaue kwa upanga.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana BWANA asema hivi, Tazama, nitakufanya kuwa hofu kuu kwa nafsi yako, na kwa rafiki zako wote; nao wataanguka kwa upanga wa adui zao, na macho yako yataona hayo; nami nitatia Yuda yote katika mikono ya mfalme wa Babeli, naye atawachukua mateka mpaka Babeli, na kuwaua kwa upanga.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana, Mwenyezi-Mungu asema hivi: ‘Tazama, nitakufanya uwe kitisho kwako wewe mwenyewe na kwa rafiki zako wote. Wao watauawa vitani kwa upanga wa maadui zao huku ukiangalia. Nitawatia watu wote wa Yuda mikononi mwa mfalme wa Babuloni, naye atawachukua mateka hadi Babuloni na kuwaua kwa upanga.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Utaniona, nikikutoa kuwa kitisho kwako wewe nako kwao wote wakupendao, maana wataangushwa kwa panga za adui zao, nayo macho yako yataviona! Nao Wayuda wote nitawatia mkononi mwa mfalme wa Babeli, atawahamisha kwenda Babeli akiwapiga kwa upanga.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana BWANA asema hivi, Tazama, nitakufanya kuwa hofu kuu kwa nafsi yako, na kwa rafiki zako wote; nao wataanguka kwa upanga wa adui zao, na macho yako yataona hayo; nami nitatia Yuda yote katika mikono ya mfalme wa Babeli, naye atawachukua mateka mpaka Babeli, na kuwaua kwa upanga.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Maana, Yawe anasema hivi: Nitakufanya ukuwe kitisho kwako wewe mwenyewe na kwa warafiki zako wote. Wao watauawa katika vita kwa upanga wa waadui zao, wewe ukiwa ukiangalia. Nitawatoa watu wote wa Yuda katika mikono ya mufalme wa Babeli, naye atawapeleka kuwa watumwa mpaka Babeli na kuwaua kwa upanga.